MSIGWA: RIPOTI YA CAG HAIZUII MIRADI YA KIMKAKATI KUENDELEA


Na Asha Mwakyonde Dodoma

WANANCHI wametakiwa kuachana na mijadala ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),kwa kuwa mijadala hiyo ina 
lenga kuharibu taswira ya nchi na kwamba miradi ya kimkakati inaendelea kutekelezwa na serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Pia vyombo vya ulinzi na Usalama vinaendelea kufanyia kazi maelekezo ya Rais Dk. Samia ya kufanya uchunguzi kwenye maeneo yote ambayo CAG ameyatolea taarifa, taasisi, kwa yoyote atakayebainika hatua zitachukuliwa.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere alitoa Ripoti hiyo  mwezi Machi Ikulu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari na baadae kupata Iftar ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan na waandishi hao jijini Dodoma Aprili 19,2023 Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -Maelezo Gerson Msigwa amesema Serikali inatumia ripoti  hiyo kama  nyenzo katika  kuhakikisha  mapungufu yote yaliyobainika yanafanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.


Msigwa ameongeza kuwa ripoti hiyo ni moja ya nyenzo ambazo Serikali inazitumia katika kusimamia rasilimali za watanzania.

Msemaji huyo  ripoti ya CAG inatumika Katika kuangalia ni maeneo gani yanahitaji kuongezewa nguvu katika usimamizi wa rasilimali za watanzania na hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.

Msigwa ameeleza kuwa  hakuna mradi wowote uliosimama huku akiwatoa  hofu wananchi kuhusu miradi ya kimkakati inayoendelea na utekelezaji wake ikiwamo ya ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 89 pamoja na ule wa mradi wa reli Morogoro -Makutopora kuwa unaendelea kutekelezwa ukiwa umefikia asilimia 93.3.

"Ripoti ya CAG imetolewa lakini haizuii kazi za Serikali kuendelea hasa katika miradi ya kimkakati, Serikali ya Rais Samia ina nia ya dhati na itahakikisha mipango yote inatekelezwa ikiwemo mabehewa ya ghorofa,mradi wa uzio wa Tembo ambao umeanza Kwa mara ya kwanza nchini na barabara ya mzungu ya Dodoma ambayo imefikia asilimia 18,"ameeleza.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU