TANZANIA NA SCJohnson ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA KUPAMBANA NA MALARIA


Na.WAF, Dar es Salaam

WAZIRI wa Afya  Mhe. Ummy Mwalimu leo Aprili 2,2023 amesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana na Kampuni ya SCJohnson ya nchini Marekani katika kupambana na ugonjwa wa Malaria nchini.

Tukio hilo limehudhuriwa na Makamu wa Rais Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Mark Martin, Balozi wa Umoja wa  Viongozi wa nchi za Afrika dhidi ya Malaria (ALMA) Mhe. Anthony Okara pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania Mhandisi Leodgar Tenga.

Tamko hilo limefikiwa kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyoifanya kwenye  makao makuu ya  kampuni hiyo yaliyopo Racine, Winscosin nchini Marekani mwezi Mei, 2022.

#MtuNiAfya

#JaliAfyaYako


Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA