TAFITI ZA KISAYANSI ZITUMIKE KULETA MAENDELEO - DKT. JINGU


 Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu akifungua Warsha ya  utengenezaji wa Vijarida Sera  vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum Juni 21,2023 Mkoani Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Makundi Maalum,Juma Samwel akizungumza wakati wa warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera  vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum, Juni 21,/2023 Mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa  uratibu na uendelezaji wa Utafiti,Tume ya Sayansi na Utafiti  (COSTECH)  Dkt Bugwesa Zabron Katale akizungumza wakati wa Warsha ya utengenezaji wa Vijarida Sera  vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum,Tarehe 21/06/2023 Mkoani Dodoma.

Baadhi ya Washiriki katika warsha ya iliyoratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) ya utengenezaji wa Vijarida Sera  vitakavyosaidia katika kutatua changamoto za Makundi Maalum,Tarehe 21/06/2023 Mkoani Dodoma.

Na WMJJWM, Dodoma

SERIKALI unaendelea kushirikiana na Taasisi za  kisayansi nchini zinazofanya tafiti mbalimbali   na  kuwa na Majibu ya kisayansi yanayowezesha kupata suluhu za kuinua  uzalishaji na vipato vya makundi Maalum.

Akifungua Mafunzo ya utengenezaji wa Vijarida sera vitakavyotatua  changamoto za Makundi Maalum, Katibu  Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ameelezea ni namna gani Sayansi na teknolojia inaweza kutumika katika kusaidia kupata majawabu yenye ushahidi ili kusaidia makundi maalum.

“Ni matarajio yetu  kikao kazi  hiki  ni makubwa kwani tunatarajia majawabu yenye ushahidi na yanatokelezeka ili kupata njia nzuri zaidi  za kusaidia  Makundi Maalum katika kuinua hali yao ya kiuchumi”Alisema Dkt  Jingu

Amesema Mazingira yanaruhusu kuja na majawabu yenye ushahidi kwani miundo mbinu ipo na imesambaa nchini ikiwemo barabara, Nishati, taasisi binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Makundi Maalum kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Juma  Samwel amesema Serikali inapambana kuhakikisha  wafanya biashara ndogondogo wanakua kiuchumi.

“Tunatamani Makundi  haya maalum yaweze kurahisishiwa mazingira ya kufanyia kazi   kwa  kushirikishwa kwa ukaribu katika masuala yanayowahusu lakini pia mamlaka husika na yanayowagusa wazalishaji  hawa wadogo kufanya nao kazi kwa  ukaribu ili kurahisisha uzalishaji wao kwa mfano  Latra kuweza kuongeza ukaribu nao ikiwemo kuwaelemisha  juu ya masuala mbalimbali”

Aidha, Mkurugenzi wa  uratibu na uendelezaji wa Utafiti,Tume ya Sayansi na Utafiti  (COSTECH)  Dkt. Bugwesa Zabron Katale amesema lengo kubwa la taasisi ni kutatua changamoto zinazokumba Jamii  katika kada mbalimbali.

“Lengo kubwa la Tume ya Sayansi na Utafiti  ni  kutatua changamoto zinazoikumba jamii kupitia tafiti mbalimbali  na kuja na masuluhisho yatauowezesha kuleta mabadiliko na maendeleo katika Taifa.Hivo kuwa na Taifa linalofanya vitu  kitaalam na si kwa mmazoe,"amesema.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI