AIR TANZANIA YAFUNGUA MILANGO KWA WAFANYABIASHARA KUOMBA NDEGE ZA 'AIR BUS' KWENDA NCHI WANAZOZITAKA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ndege nchini la Air Tanzania Mhandisi. Ladislaus Matindi (kushoto)akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo alipotembelea banda la Air Tanzania.

Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

WAFANYABIASHARA wametakiwa kupeleka mipango yao ya kubebewa mizigo  katika uongozi wa Shirika la ndege la Air Tanzania ambapo itawasikiliza kulingana na matakwa ya wafanyabiashara hao ya kupelekewa mizigo wanapohitaji iende.

Akizungumza Julai 02,2023 ,kwenye Banda la Air Tanzania katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF),maarufu Saba Saba, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ndege nchini  la Air Tanzania Mhandisi. Ladislaus Matindi amesema Wafanyabiashara wengi wa Tanzania walio na mahusiano makubwa ya kibiashara na nchi za Falme za kiaraabu wameshaanza safari kwa kutumia air bus.

Akizungumzia ndege za 'Air bus' amesema kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na changamoto na kwa sasa wanatarajia ifikapo kati kati ya mwezi huu ndege mbili zitakuwa zimerudi na kufanya idadi ya ndege hizo za air bus kuwa tatu na kwamba mwezi wa nane wanatarajia kuipokea nyingine.

Mkurugenzi huyo amesema ifikapo mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu ndege hizo zitakuwa zimeshaanza kutoa huduma.

Ameongeza kuwa kuwapo kwa ndege hizo, nguvu yao ya kutoa huduma itakuwa imeongezeka na kwamba wanajua mahitaji ni makubwa ambapo kwa sasa wanandege tatu.

Mhandisi Matindi ameeleza kuwa wamekuwa wakishiriki maonesho hayo kwa kushirikiana na wadau wengine ambapo kwa sasa waameamua. kushiriki wenyewe.


Mhandisi Matindi amesema kuwa lengo kubwa ni  kujitangaza katika maonesho hayo na wananchi waweze kuwafahamu na  kuwafahamu wateja wao ambao ni wananchi hao.

"Tumekuwa tukishiriki maonesho haya kwa kushirikiana na wadau wengine lakini tumeamua kushiriki wenyewe kwa mara ya pili kuwa na banda letu, kwa kuwa ni muhimu kwa sisi kujitangaza,kuonesha bidhaa zetu, kusikiliza wananchi wanasemaje," amesema.

Mkurugenzi huyo amesema wameendelea kuongeza idadi ya ndege za abiria  ambapo kwa sasa wanandege 12  na wanatarajia kuongeza nyingine 3.

Akizungumzia Mkoa wa Dodoma kuhusu usafiri huo ameeleza kuwa juhudi za kuweka taa ili ndege ziweze kwenda usiku zinaendelea na kwamba ifikapo Novemba mwaka huu zitakuwa zimekamilika zitawapa wigo mpana zaidi watumiaji na kuchagua ni muda gani anaweza kusafiri.

Amefafanua kuwa Dar es salaam itabaki kuwa Jiji la biashara hivyo mfanyabiashara atachagua ni muda gani anaweza kusafiri kurudi akiwa amemaliza kufanya biashara zake.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI