UDOM KUJA NA PROGRAMU MPYA YA KUMDHIBITI MWANAFUNZI WA FANI YA AFYA KWENYE MAFUNZO


Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

CHUO kikuu cha Dodoma (UDOM), kinatarajia kukamilisha mfumo, programu ambao itakuwa onesha wakati wote mwanafunzi anayesomea fani ya daktari na nesi akiwa katika mazoezi ya vitendo kwenye Hospitali.

Kupitia programu hiyo  mwanafunzi atajiandikisha na mwalimu na msimamizi wake chuoni anajua mwanafunzi huyo anachokifanya  ikiwamo kujua yupo kwenye wodi gani.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 02,2023  kwenye Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), maarufu Saba Saba, Makamu Mkuu wa Chuo Cha UDOM, Profesa. Lughano Kuziluka ameeleza kuwa Programu hiyo inaonesha ni kitu gani mwanafunzi anatakiwa kukifanya akiwa kwenye kitanda anachomuhudumia mgonjwa.

Prof. Kuziluka amesema  uzuri wa programu hiyo inawarahisishia kujua kila mwanafunzi anapohudhuria mafunzo hayo lazima awepo anapotakiwa kuwepo kwa wakati unaotakiwa.

Aidha amesema kuwa chuo hicho kina programu ya utunzaji wa kumbukumbu za afya, namna ya kufuatilia wanafunzi ambao wanasoma masomo ya udaktari, nesi wanapokuwa katika mafunzo yao hospitalini.

"Chuo cha UDOM tupo hapa kwa sababu ni wadau wakubwa wa maonesho haya tumekuja kuwafahamisha Watanzania kuwa Chuo chetu  ni moja ya Vyuo vikuu vikubwa nchini Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki  mtu akiingia atapata programu zetu zote," amesema.

Ameongeza kuwa kumbukumbu za kwenye karatasi wakati mwingine ufuatiliaji wake  unakuwa mgumu ambapo programu hiyo inatoa taarifa zote za mwanafunzi na kuwasaidia walimu kujua mwanafunzi huyo anafanya nini.

Pia amesema chuo hicho kinafanya Utafiti,Ubunifu na Uvumbuzi zikiwamo za kutunza mazingira kwa kutengeneza mapambo ya nyumbani kupitia chupa zinazotupwa lengo likiwa ni kupunguza uchafu unaoharibu mazingira.

Prof. Kuziluka amebainisha kuwa ni matumizi mazuri ya rasilimali ambazo zimetumika kukwekea vimiminika na baadae kutupwa na kuchafua mazingira.

"Tunatamani kuwa na nchi yenye mazingira mazuri na watu wanaishi katika mazingira safi hivyo nawakaribisha Watanzania kuja kuona Ubunifu huu wa chupa na kuzinunua kwa ajili ya kuzitumia nyumbani," amesema Prof. Kuziluka.


Amefafanua kuwa vitu vingine wanavyoonesha katika maonesho hayo ni namna ya kuendesha kilimo kwa kutumia  vitalu nyumba'Green Houses'.

Prof. Kuziluka amesema katika maeneo mbalimbali changamoto inayokuwepo ni kujua mazao yaliyopo yanapata unyevunyevu, joto la kutosha na maji ya kutosha huku akisema wataalam wao wamefanya Utafiti na kujua mfumo ambao wakati wowote unawezakusaidia kupunguza au kuongeza, joto, unyevunyevu kulingana na mahitaji ya mazoa husika.

Akizungumzia programu za masomo wanayoyatoa chuoni hapo amesema kuwa chuo kina toa programu kuanzia ngazi ya shahada, shahada ya kwanza, shahada za umahiri hadi shahada za Uzamili na Uzamivu na kwamba wapo wataalam wanaotoa taarifa hizo kwa ufasaha. 

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI