VETA MIKUMI YATAMBULISHA MASHINE YA KUCHAKATA MAGOME YA MIGOMBA NA KUPATA NYUZI SABA SABA


Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

VIJANA wameshauriwa hasa wale wanaoiona Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA),kupitia Vyuo vyake kama sehemu ya kuwapotezea muda  na badala yake wavitumie vyuo hivyo kuweza kupata ujuzi wa kudumu katika maisha yao kwa kuajiriwa au kujiajiri.

Akizungumza Julai 02,2023 kwenye Banda la VETA katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), Mwalimu Msaidizi  wa mafunzo kutoka Chuo cha VETA ambaye pia ni mbunifu wa mashine ya kuchakata magome ya mgomba na kupata nyuzi 'Banana Fibre Extractor ' Peris  Shao, amesema kuwa amebuni mashine hiyo kwa lengo la kuwa rahisisishia wajasiriamali kupata nyuzi hizo kwa urahisi zaidi. 

Amefafanua kuwa kamba iliyotengenezwa kwa kutumia magome ya mgomba inatumika kutengeneza kamba ambayo inafunga meli baharini wakati inatia nanga huku akisema inavumilia maji ya chumvi tofauti na iliyotengenezwa kwa katani.

"Nimebuni mashine ya kutengeneza nyuzi kwa kutumia magome ya migomba ambazo zitaenda kufanya kazi mbalimbali ikiwamo kutengeneza kamba ambazo zinatumika kutengeneza kamba za kufungia mifugo pamoja na mikoba ya akina mama," amesema.


Ameongeza kuwa amebuni mashine hiyo baada ya kuona mgomba una malighafi ambayo inaweza kutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali mbali na kutumika kwa ajili ya chakula ndizi zake.

Mbunifu huyo ameeleza kuwa wao kama Chuo cha VETA Mikumi wamebuni mashine hiyo ili kumrahisishia mjasiriamali kuweza kutumia mashine kwa ajili ya kuongeza kipato chake kwa urahisi zaidi.

Amesema baada ya kuchakata magome ya mgomba mabaki yake yanatumika kama mbolea ya kupandia maua na mazao shambani.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI