Na Asha Mwakyonde Dar es salaam
CHUO cha Mafunzo Ya Ufundi Stadi(VETA),Dar es salaam kimebuni mashine, Mtambo wa maji 'Water Distiller Machine ' lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi katika uzalishaji wa bidhaa za mafuta.
Pia vijana wameshauriwa kuwa na ubunifu utakaowasaidia katika maisha yao ambao ubunifu huo ndio utakaowasaidia.
Akizungumza Julai 02,2023 ,kwenye banda la Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA),katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF),maarufu Saba Saba, Mwalimu wa fani ya Maabara kutoka chuo cha VETA Dar es salaam Ally Issa amesema Mtambo huo ni kwa ajili ya kutoa mafuta kutoka Kwenye mabaki ya matunda yakiwamo ya chungwa pamoja na tangawizi ambayo ni dawa tiba.
Issa ameeleza kuwa matambo, mashine hiyo inaenda kuwagusa moja kwa moja wakulima wa matunda, mazao ya mboga mbonga.
Amefafanua kuwa kuyapata mafuta hayo ni gharama kubwa ambapo milimita 30 inauzwa kwa shilingi 60,000 na kwamba mabaki ya yanayotokana na matunda yanafaida kubwa kiuchimi.
Issa amefafanua kuwa mashine hiyo ilitengenezwa kwa kipindi cha mwezi mmoja ambapo imegharimu milioni 1.5 na kwamba ikipelekwa kuuzwa sokoni itauzwa zaidi ya milioni 2.
Akizungumzia Fani ya Maabara amesema inatolewa katika Vyuo vinne vilivyopo katika mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Manyara pamoja na Pwani lengo ni kuwaandaa wanafunzi ili waweze kuwa mahiri na kufanya kazi sehemu mbalimbali zikiwamo za viwandani.
Amesema kuwa wameangalia ni changamoto gani jamii inakutana nazo katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora unaotakiwa.
0 Comments