CHUO CHA MIPANGO CHAJIKITA KUWAANDAA WANAFUNZI KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI


 Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam

SERA za uwekezaji hapa nchini inahitaji mchango mkubwa wa taasisi za Elimu ya juu katika kuandaa na kutoa Wahitimu  walioandaliwa  vizuri kulingana na mahitaji ya soko.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam Julai 03 2023 katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo "Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,"
na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi za Taaluma wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dkt. Yohana Mgale alipoluwa anaongea na waandishi wa habari waliotembelea banda la Chuo hicho lilikwenye Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Mgale ameeleza kuwa Chuo  cha Mipango kwa kutambua hilo  kimejikita katika kuwaanda Wahitimu wa Chuo hicho ili wame na stadi stahiki za kuwafanya kuwa mahiri katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Tunawafundika kufanya tafiti  katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi , ikiwemo kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili wananchi hasa wa vijijini, uandaaji wa mipango mkakati, kufanya ufiatiliaji na tathimini ya miradi ya Maendeleo. 


Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Chuo cha Mipango kimejipanga kutoa mafunzo yanayowajengea wanafunzi uwezo kwa vitendo na nadharia lengo likiwa ni kuzifikia fursa zinazotokana na wawekezaji kwa kujikita kuwekeza katika rasimali watu.

 "Ili kutumia fursa zinazoletwa na uwekezaji ni muhimu kama taifa kuwa na rasilimali watu iliyoandaliwa vizuri kulingana na mahitaji ya sasa.

Mafunzo yetu yanafuata mfumo wa umahiri na weledi ambapo mwanafunzi anajifunza nadharia na vitendo," ameeleza Dkt. Mgale.

Ameongeza kuwa wanawaandaa wanafunzi kuweza kujiajiri kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuendeleza bunifu za wanafunzi kupitia Kituo cha Ubanifu na Ujasiriamalia kilichopo chuoni hapo.

Dk. Mgale amefafanua kuwa mbali ya kutoa mafunzo ya muda mrefu vile vile Chuo kimejikita katika kuendesha mafunzo ya mfupi katika fani mbalimbali kama uandaaji wa mipango mkakati, kuandaa bajeti, uandaaji na usimamizi wa miradi, tathimini ya miradi, usimamizi wa vihatarisi.

Amewataka wananchi kutembelea banda la Chuo hicho lililopo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango huku akisema kwamba kwa wale watakao kosa nafasi ya kuwatembelea kwenye Maonesho ya 47 ya Sabasaba wanaweza kuwatembelea katikati Maonesho ya 18 ya Vyuo vya Elimu ya Juu yanayoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) katika ya mwezi huu Julai. Maonesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam. 

" Tunatumia Maonesho kama haya kubadilishana uzoefu na wadau wetu na pia kupata mrejesho na huduma zetu . Kwa mantiki hiyo tumepanga kushiriki Maonesho ya Wakulima na wafugaji maarufu Nanenane amabapo tutakuwa Viwanja vya Kanda ya Kati kule Dodoma, Nyakabindi Kule Mwanza, na John Mwakangale kule Mbeya ambako yatafanyika kitaifa. Aidha, tutashiriki Maonesho ya Nne ya Elimu Zanzibar yanayoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amari ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mapema Mwezi Agosti, 2023" alisema na kuongeza "hii ni fursa kwa wanafunzi wanaohitaji kujiunga na Chuo chetu kututembelea katika Maonesho hayo ilikupata huduma ya kujiunga na Chuo". Dkt. Mgale amedokeza kuwa wahitaji wanaweza kuomba kudahiliwa kupitia tovuti ya Chuo kwa kupitia link *oas.irdp.ac.tz*

Amefafanua kuwa maombi kwa programu zote za kuanzia Astashahada hadi Shahada za Umahiri ni bure. 


Dkt. Mgale amesema chuo hicho kinatoa kozi za Astashahada (certificate) ambapo wana programu 7, Stashahahada,
 (Diploma) programu 7, huku akibainisha kwamba Astashahada na Stashahada zipo katika fani za Maendeleo Vijijini (Rural Development),Usimamizi wa Maendeleo
(Development Administration and Managemant), Maendeleo Vijijiji
(Rural Development), Upimaji Ramani (Geomatics), Mipango Miji
(Urban Planning), Fedha na uhasibu (Accounting and Finance) na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). 

Dkt. Mgale ametaja sifa za kujiunga na programu za Astashahada  ni  ufaulu wa angalau masomo manne (4) pasipo masomo ya dini, na kwa upande wa  Stashahada meombaji anapaswa kuwa aidha na Astashahada ya  ufaulu wa G.P.A ya 2.0  kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na serikali  au "Principal"  pasi moja na "Subsidiary" moja katika matokeo ya   Kidato cha Sita. 

Dkt. Mgale amesema ada zao ni rahisi  na zinahimilika kwa watanzania wa hali zote.  "Mbali ya ada zetu kuwa nafuu  sana pia tumetengeneza mazingira rafiki za ulipaji wa ada hiyo ambayo hulipwa kwa awamu nne kwa mwaka.


Kwa mujibu wa Dkt. Mgale Chuo pia kinaendesha programu kumi na moja za Shahada ya Kwanza katika fani za Mipango ya Maendeleo ya Mikoa  (Regional Development Planning); Usimamizi wa Mazingira (Environmental Planning and Management); Usimamizi wa Rasilimali watu (Human Resourcee  Management); Idadi ya Watu na Mipango ya Maendeleo (Population and Development Planning); Mipango ya  biashara (business Planning); Maendeleo ya Jamii (Community Development); usimamizi wa miradi (Project Planning and Managent); na Uchumi (Economics).

Nyingne ni  Mipango Miji (Urban  Planning);  na Fedha za Maendeleo na Mipango ya Uwekezaji (Development Finance and Investment Planning) zote zikiendeshwa kwa muda wa   miaka mitatu isipokuwa fani ya Mipango Miji ambayo ni miaka minne.

Dkt. Mgale anamalizia maelezo take kwa kutaja kundi la tatu la programu ambalo ni Shahada za Umahiri na Stashahada za Uzamili ambazo nazo zimejikita katika  fani za mipango, usimamizi wa miradi, uchumi wa maendeleo, usimamizi wa mazingira, maendeleo ya jamii, usimamizi wa rasilimali watu, pamoja na afya na usafi wa mazingira. Sifa za kujiunga ni walau ufaulu wa  GPA 2.7 kutoka Chuo kinachotambuliwa na serikali kwenye fani husika," ameeleza.




Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI