Na Asha Mwakyonde Dar es salaam
SERIKALI ipo kwenye hatua ya kukamilisha mazungumzo na wawekezaji kwenye eneo la Mradi wa kuchakata na kusindika gesi Asilia (LNG),ambapo manufaa makubwa yanayotarajiwa kwa wananchi kupitia mradi huo.
Pia serikali inaendelea na jitihada za kuifanya nishati jadidifu kuwa nishati ya umeme ambayo ni mbadala wa mabadiliko ya hali ya hewa katika uzalishaji umeme.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam Julai 03,2023 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alipotembelea banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF), maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,"amesema
mradi wa LNG ndiyo mradi ambao utaiwezesha Tanzania kuuza gesi nje ya nchi na kunufaika kutoka katika rasilimali hiyo ambayo inapatika katika maeneo ya Mtwara na Lindi.
Ameyataja manufaa hayo kuwa ni kuanza kunufaika na gesi ambayo imegunduliwa muda mrefu na haijaweza kutumika kwa kiasi kikubwa ambapo matumizi ya gesi hiyo mpaka sasa ni kuzalisha umeme, ambao zaidi ya asilimia 64 ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na gesi asilia.
Katibu huyo ameongeza kuwa dunia inaanza kufikiria kuhama kwenye matumizi ya nishati chafu inayozalisha gesi ya ukaa kwa wingi na kuhamia kwenye gesi safi zaidi.
"Tanzania tuna bahati tuna gesi ambayo inaviwango vidogo vya hewa ukaa, lakini pia serikali ilikuwa na mazungumzo na wawekezaji kwenye eneo la mradi wa LNG na mazungumzo hayo yamefika mwisho na sasa tunaenda kupata gesi safi na ya uhakika", Mhandisi Mramba.
Aidha, Mramba amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali Serikali inaangalia katika kuzalisha umeme kupitia chanzo cha Jotoardhi ambapo katika maeneo ya Songwe, Mbeya Wilayani Tukuyu, ziwa Natroni mkoani Arusha na maeneo mengine katika Mkoa wa Pwani.
0 Comments