Na Asha Mwakyonde,Dodoma
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),imekutana na kujadili mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),ambapo imeonesha kutokuridhika kutokana na kupata nakisi zaidi.
Pia kamati hiyo itawasilisha kwenye ofisi ya Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson kwa ajili ya kuona njia bora zaidi ya kuishauri serikali katika kuhakikisha mfuko huo
Akizungumza jijini Dodoma leo Agosti 17,2023 Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jerry Silaa amesema mfuko huo umekuwa ukipata nakisi zaidi ya mwaka ambapo mwaka 2020 ulipata nakisi ya bilioni 49, na mwaka unafuata wa mwaka 2021 ulipata nakisi bilioni 109 .
Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa mwaka wa fedha ulioisha 2021/2022 kutokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyowasilishwa mwaka huu umepata nakisi bilioni 204.
Amesema kuwa mtaji wa mfuko huo umepungua kutoka trilioni 1 hadi zaidi ya bilioni 700 huku akisema hali hiyo haileti sura nzuri katika uhai wa mfuko huo.
"Nadhani ni suala ambalo linafahamika mfuko huu umekuwa ukipata nakisi zaidi ya mwaka ambapo mwaka 2020 ulipata nakisi ya bilioni 49, na mwaka unafuata wa mwaka 2021 ulipata nakisi bilioni 109 na mwaka jana tulikutana nao Agosti 2022 na kuwapatia maelekezo ya mambo ambayo yangefanyika matatizo yangekuwa yapungua," ameeleza.
Ameeleza kuwa wanatarajia sheria ya bima hiyo ikipita bungeni NHIF ndio itakuwa mtekelezaji wa kuweza kusaidia wananchi kupata huduma ya afya.
Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ina mkakati wa kutengeneza bima ya afya kwa watu wote.
Slaa amesema utendaji wa Mfuko huo na jukumu walilonalo ambapo kwa sasa wanawanachama wameongezeka kwa kipindi cha Juni 2020 hadi Juni 2022 inaonesha ufanisi kama unaanza kusinzia.
Amesema kuwa kamati hiyo imekutanoa na uongozi wa Mfuko huo na kufanya majadiliano marefu kuliko vikao vingine.
Amesema yapo mambo ambayo kamati hiyo itawasilisha kwenye ofisi ya Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson kwa ajili ya kuona njia bora zaidi ya kuishauri serikali katika kuhakikisha mfuko huo unakua na aina fulani ya utendaji ambao wataona miaka ya fedha ijayo nakisi hizo zinaondoka.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa kuna jambo kubwa la umakini katika usimamizi wa rasilimali fedha na mifumo inayotumika katika usimamizi huo.
Amefafanua kuwa kuna mambo mengi yanafanyika katika mfuko huo huko mitaani unaendelea watu kutibiwa na bima ambazo sio za kwao wengine hawajiungi na Mfuko huo.
0 Comments