DC SHEKIMWERI ASISITIZA KUUNDWA TIMU YA UFUATILIAJI ANWANI ZA MAKAZI

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri,  amesisitiza kuundwa kwa  Timu ya ufuatiliaji na tathmini ya zoezi la Anwani za Makazi  ili kufanikisha azma ya Serikali ya kila Mtu  kutambulika kirahisi mahali anapoishi kwa lengo la kufikiwa na  huduma za Kijamii kwa haraka.

Pia ametoa wito kupitia vikao vya kisheria ikiwamo Mabaraza ya madiwani kupewa muda wa kuwasilisha elimu ya suala hilo na wajibu wao wa kuhamasisha wananchi kujisajili na mfumo wa anwani za makazi.

Shekimweri ameeleza hayo leo Septemba 14,2023 Jijini Dodoma ,wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Kuwajengea  uwezo kuhusu Mfumo wa anwani za Makazi kwa MaafisaTarafa,Maafisa Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa pamoja  na Maafisa Watendaji wa Mitaa wa Jiji la Dodoma ambayo  yameandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano naTeknolojia ya Habari .

Ameeleza kuwa kwa  sasa imekuwa ni rahisi kuita gari la kukodi (Uber) ukaonesha eneo unapokwenda na huduma hiyoikakufikia, hivyounaweza kuita huduma ukiwa nyumbani kwako
DC. Shekimweri.


Kwa Upande wake Mratibu wa anwani za Makazi Kitaifa,Mhandisi Jampion Mbugi ameeleza kuwa  lengo la Mafunzo hayo ni kulifanya Jiji hilo kuwa la mfano katika kutekeleza zoezi hilo.

Ameongeza kuwa dhamira ya Wizara ni kuhakikisha Dodoma inakuwa ya mfano na kuwa chachu kwa halmashauri zingine kuja kujifunza namna ya kufanikisha utekelezaji wa mfumo huo.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU