SACP MISIME AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU MBILI


Na, Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) David  Misime amefunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa,Wakaguzi na Askari wa Polisi kutoka Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma.

SACP Misime amewaeleza Askari hao kuwa mafunzo hayo ni mfululizo  wa mafunzo yanayotolewa kwa Askari  katika Vyuo ndani ya nchi, nje ya nchi na kazini kwa lengo la kuwabadilisha kifikra (mindset change) ili kutoa huduma bora kwa jamii.

SACP Misime amefungua mafunzo hayo Septemba 20, 2023   katika ukumbi wa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Yalifanyoka kwa engo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu.

"Mkibadilika kifikra na kuhudumia wananchi kwa Nidhamu,Haki,Weledi na Uadilifu mtakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya wananchi kifua mbele na kwa kutumia Falsafa ya Polisi,wananchi waka waamini na kuongeza imani kwa Jeshi la Polisi ili waoneshe ushirikiano katika kubaini na kuzuia uhalifu".Amesema Misime.

Pamoja na hayo, Misime amewapongeza Askari kwa kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kazi kubwa wanayofanya huku akiwataka kwenda kuyafanyia kazi yale waliojifunza ili wananchi waweze kuona mabadiliko ya kifikra na  kiutendaji kulingana na mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi.

Awali Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto  kutoka  Makao  Makuu  ya Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman amewasisitiza Askari wa Kike kuzingatia maadili, kutunza familia, kujijengea  uwezo wa kujiamini, kuwa wasafi na kuachana na vyanzo vyote vya mawazo kama vile kujiingiza katika mikopo isiyo na msingi ambayo muda mwingi huwapelekea kuwa ni watu wenye mawazo.

Hata hivyo, ACP Faidha Suleiman ambaye ni mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Makao makuu ya Polisi amewataka askari kuhakikisha wanafuata na  kutekeleza miradi ya Polisi Jamii katika majukumu yao ya kila siku kwani miradi hiyo inagusa kila kitengo cha Jeshi la Polisi. 

Alisisitiza katika kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto katika familia zao na jamii kwa ujumla ikiwemo wao wenye kutokujifanyia ukatili. 

Naye Mkuu wa Dawati la mtandao wa Polisi wananwake (TPF Net) Makao Makuu ya Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Eva Stesheni amewataka askari kujifunza namna ya kuandika ripoti ya kazi zao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi  pamoja na kuwasidia katika utunzaji wa kumbukumbu za nyaraka kwa kuwa na mpango kazi ulio mzuri ilikufikia malengo sahihi , Kuwasilisha taarifa, mawazo  na kuendeleza ujuzi  hasa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto.

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto  mkoa wa Dodoma mkaguzi wa Polisi  Teresina  Mdendemi amewataka askari kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje  kwani kupitia utoaji wa huduma bora huweza kusaidia kurahisha utendaji kazi wa kila siku na kusaidia katika kupambana na vitendo vya kihalifu hususani unyanyasaji wa kijinsia.

"Tutambue na  kufahamu aina ya wateja  Pamoja na  hisia zao pia tuwe  na moyo wa kusamehe kwa lengo la kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na Jamii  katika kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia  na ukatili dhidi ya watoto   na vitendo vyote vya kihalifu".Amesesisitiza Mdendemi.

Kwa upande wake Mkuu wa  Dawati la Jinsia  mkoa wa Pwani  Mkaguzi  Msaidizi wa Polisi  Eliezer  Hokororo  amezungumzia  Faida na athari ya afya ya akili na kusema kuwa ukiponya akili umeponya maisha yako yote maana akili ni mfumo mzima maisha ya mwanadamu na  

kewamba watu wengi wameathirika na ugonjwa wa Sononc ambao umetokana na kukosekana na ubora wa afya ya akili na   kuchangia kuharibu Fikra, Hisia na Matendo ya mtu kutokana na kutokuwa na afya bora ya akili na mara nyingine kushindwa kabisa kutatua changamoto wananzokutana nazo.

Aidha Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Njombe Mkaguzi msaidizi wa Polisi Wilfred Willa  aliwataka askari wa kike kutambua na kuzingatia wajibu wao kwa kuihudumia vyema Familia na jamii huku akisema mwanamke anapaswa kuwa kioo na mwenye tabia njema maana ndiye nguzo kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI