UJENZI WA MINARA WAFIKIA ASILIMIA 90, WATANZANIA MILIONI 15 KUNUFAIKA


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote ( UCSAF), umesaini mikataba ya kupeleka huduma za mawasiliano  maeneo ya vijijini  katika ujenzi wa minara ya mawasiliano kwenye Kata  zaidi ya 1900 ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 90.

Pia Watanzania wapatao milioni 15 watapata huduma za mawasiliano kupitia ushirikiano wa serikali chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza jijini Dodoma  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa UCSAF, Justina Mashiba ameeleza kuwa Ujenzi wa minara hiyo umebakia asilimia 10 kukamilika.

Mtendaji huyo ameongeza kuwa kazi kubwa imefanyika ya ujenzi wa minara katika maeneo ya vijijini pamoja na miradi mingine na kwamba  wanaenda katika maeneo ambayo ni magumu kufikika.

 "Serikali iliwatoa waliokuwa wakiishi Ngorongoro.na kuwapeleka kijiji cha Msomera kilichopo wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, sisi kama mfuko wa UCSAF wamefanya miradi mitatu katika kijiji hiki," amesema.

Amefafanua kuwa wamejenga mnara katika kijiji cha Msomera kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),ambao ndio
waliojenga mnara huo.


"Nawashukuru watoa huduma za mawasiliano kwa sababu wote wamepeleka huduma zao kupitia mnara wa TTCL kwa kwenda kuweka vifaa vyao,' ameongeza.

"Ushirikiano huu wa UCSAF pamoja na watoa huduma za mawasiliano ni moja ya mifano mizuri ya mahusiano kati ya sekta binafsi na serikali, huu ni mfano ambao upo hai, niwaombe kuendelea kushirikiana ili azam yetu ya Tanzania yote inapata huduma za mawasiliano" ameeleza.

Amesema eneo hilo la Msomelo usikivu unapatikana huku akishuru juhudi za serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote.

Mtendaji huyo emebainisha kwamba katika ziara yao na Waziri Nape kwenye kijiji hicho walielezwa kuwa kuna ujenzi wa nyumba nyingine takribani 5,000 kwa wanaoendelea kuhamia kutoka Ngorongoro.

"Kwa sasa wanahamia kijiji cha Mkababu na inaonekana ni eneo 
lenye changamoto kubwa ya mawasiliano kwa sababu hapakuwa na mtanzania aliyekuwa anaishi, sisi kama UCSAF jukumu letu ni kuhakikisha tunapeleka huduma kwa kushirikiana na TTCL chini ya Mhandisi Peter Ulanga kwenda kupeleka huduma za mawasiliano," ameeleza.

Amefafanua kuwa mradi huo upo katika hatua za mwisho ambapo unakamilika kabla ya Watanzania hao hawajahamia katika kijiji cha Mkababu na kwamba watakapofika watakuta huduma za mawasiliano zipo.

Mtendaji Mkuu huyo amesema kuwa huduma ya mawasiliano inayopatika ni ya 4G na kwamba UCSAF inatumia Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kuhakikisha wanafuanzi wao na wanajamii wanaweza kupata elimu ya TEHAMA hiyo kupitia vifaa mbalimbali.


"Shule ya msingi Samia Suluhu ni miongoni mwa shule zilizonufaika na mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule zetu za Umma na tumepeleka kompyuta, projekta na printa na pia tumeshirikiana na wenzetu wa TTCL tumepeleka Mkongo wa Taifa," amesema.

Mtendaji huyo amebainisha kuwa shule hiyo ina darasa zuri ambalo wanatumia kufundishia watoto wanaotoka katika jamii ya kimasai ambapo watapata taarifa mbalimbali kupitia TEHAMA.

"Nameshukuru Waziri wetu wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye pamoja na Wizara yetu kwa ujumla, Bodi ya Wakurungenzi na Menejimenti ya mfuko na wafanyakazi wake kwa namba ambavyo tunashirikiana kuhakikisha jukumu ambalo tumekasimiwa la kupeleka huduma za mawasiliano vijijini tunalitekeleza kama linavyotakiwa kutekelezwa," amesema.

Mfuko huo ni taasisi ya serikali ambayo imekasmiwa  jukumu la kupeleka huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini kupitia sheria ambayo imeanzisha taasisi hiyo ya sheria namba 11 ya mwaka 2006 ambapo shughuli zake zilianza mwaka 2009.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA