WADAU SEKTA YA UJENZI KUKUTANA KESHO, KAMPUNI 120 KUTOKA NJE NA NDANI YA NCHI


DAR ES SALAAM

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Maonesho ya Dar Constructions Expo kwa lengo la kujifunza teknolojia mpya itakayopatikana katika sekta ya ujenzi

Hayo amesemwa leo Oktoba 10,2023  na  Mkurugenzi na Muandaaji wa Maonesho hayo Bw. Deogratius  Kilawe , alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee  jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa  Maonesho hayo  yana lengo la kuwakutanisha kwa Pamoja Wadau wa Sekta ya Ujenzi na kujadili njia mbalimbali zitakazosaidia kuinua Sekta hiyo pamoja na kukuza Mahusiano na kujipatia Wateja wa Bidhaa zao.


 Pia amesema Maonesho haya   yanatarajiwa kuwa ni ya siku Tatu kuanzia  Tarehe 11- 13  Oktoba 2023  na kufanyika katika  Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dae es salaam.

 Aidha Bw. Kilawe amesema kuwa, huu ni msimu wa 7 wa  Maonesho ya Dar Constuctions Expo na   yanajumuisha zaidi ya  Makampuni  120 kutoka nje na ndani ya Tanzania pia yanatarajiwa kuwa yenye kuleta Tija na Mapinduzi katika sekta ya ujenzi  na kukuza na

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI