RAIS MWINYI KUWA MGENI RASMI CRDB BUNGE GRAND BONANZA, WANANCHI WAKARIBISHWA


 Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

BUNGE la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kushirikiana na CRDB Bank limeandaa Bunge frendi bonanza litakalo fanyika tarehe 22/6/2024.

Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Mh. Festo Sanga ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma huku akibainisha kuwa mgeni rasmi katika michezo hiyo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Hussen Ally Mwingi.

Amesema CRDB BUNGE Grand Bonanza linalodhaminiwa na Benki ya CRDB linataraji kufanyika 22, juni 2024 amesema dhamira ya Bonanza hilo ni kuimarisha zaidi mahusiano kwa watumishi wa bunge na wabunge,Taasisi za serikali na bunge pamoja kuhimiza suala la afya.

"Umuhimu wa Bonanza hilo nikuimarisha uhusiano mzur Kati ya wa Bunge na watumishi Kwa pande zote za muungano, " Amesema Mwentekiti huyo

Kwa upande wake mkurugenzi WA mawasiliano Tuliether Mwampamba kutoka CRDB Bank amesema Bank hiyo imekuwa ikishirikiana Kwa ukaribu na wabunge ambapo wamekua wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za kibank Kwa wabunge na kudhamini mabonanza ya kimichezo yenye lengo la kuimarisha afya na katika bonanza Hilo wametoa Zaid ya milion 200.

" Benki ya CRDB imeendelea kuonesha ushirikiano na bunge katika sekta ya michezo pamoja kupeleka maendeleo katika majimbo, " Ameeleza .

Vile vile Bank ya CRDB wamekabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bunge Spots Club ikiwa ni Mipira, Jezi na makombe kwa ajili ya shughuli ya kesho katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Vifaa hivyo vimegharimu ujumla ya fedha za kitanzania shilingi milioni 85 ambapo ujumla kuu ya ya udhamini wa bonanza hilo ni shilingi Milioni 266.7 zinazojumuisha na maandalizi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI