SERIKALI NA WAFANYABIASHARA WAAZIMIA HOJA 15 KATI YA 41 KUSITISHA MGOMO


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akutana viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), kuzungumzia madai na hoja takribani 41 ambazo wafanyabiashara waliziwasilisha serikalini ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ambapo kati ya hoja hizo 15 wameafikiana kuzizimamia.

Hatua hiyo inatokana na kikao cha siku mbili baina ya Waziri Mkuu Majaliwa viongozi wa wafanyabiashara hao ambacho kilikuja na maazimio ya kusimamia hoja hizo 15.

Akizungumza leo Juni 27,2024 jijini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Thobias Makoba ameeleza kuwa wameafikiana kusimamia maazimio 15 ambayo ndani yake serikali imetoa maagizo yafuatayo kwa taasisi husika.

Msemaji huyo ametaja baadhi ya maazimio hayo kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kusitisha mara moja mazoezi yote ya kamata kamata pamoja na kusitisha mazoezi mengine yote ya ufuatiliaji wa risisti za EFD katika maeneo yote nchini hadi mwezi Agosti, 2024.

Amesema pamoja na kusitishwa huko wafanyabishara wanahimizwa kuelendelea kutoa risiti za mauzo na kwamba TRA inaagizwa kuweka mfumo mzuri utakaowezesha utoaji wa nyaraka muhimu za manunuzi wakati wa uingizaji wa bidhaa nchini kuanzia Julai, 2024. 

"Utekelezaji wake utawekewa utaratibu mzuri kwa kushirikisha wadau wote muhimu,"ameeleza Msemaji huyo.

Makoba ameyataja maazimio na maagizo mengine kuwa ni serikali imeelekeza Wizara ya Fedha kuratibu zoezi la kufanya uchambuzi, tathmin na mapitio ya mfumo mzima wa utozaji na ukusanyaji pamoja na viwango vya Ushuru wa Huduma (Service Levy) pamoja na kushauri njia mbadala ya utozaji itakayo kuwa rafiki zaidi kwa wafanyabiashara ili kulinda mitaji na ukuaji wa biashara nchini.

"Kuhusu wafanyabiashara kutoka nje ya nchi, Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) na mamlaka zingine husika itaendelea kuimarisha ukaguzi wa vibali vya kazi kwa wageni ili kuhakikisha kuwa wamiliki wa vibali hivyo wanafuata masharti ya vibali hivyo kwa mujibu wa Sheria za nchi," amesema.

Aidha amefafanua kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wanaokiuka Sheria, Kanuni, Taratibu na masharti ya vibali vya ajira ikiwa ni pamoja na kuwafukuza nchini na waajiri husika kuchukuliwa hatua za kisheria

Makoba amesema kwa maslahi mapana ya nchi serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wote kama ambavyo Mheshimiwa amekuwa akisisitiza katika uongozi wake.

Ameeleza kuwa kutokana na maazimio haya na maagizo ya serikali, pande zote mbili zimekubakiana hali ya biashara kote nchini kuendelea kama kawaida ili kuwapa watanzania huduma wanazostahili.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI