WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MICHEZO KUDUMISHA MUUNGANO


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanziba Hemed Suleiman Abdullah Amewataka watanzania kutumia michezo kudumisha Muungano amani na mshikamano kwani Ndio Tunu ya Taifa la Tanzania.

Ameyasema hayo jijini hapa Juni 22, 2024 wakati akifunga Bonanza la wabunge lililoandaliwa na Benki ya CRDB ambapo alisema watumishi wa serikali na Wabunge walitumie Bonanza hilo kuimarisha afya zao.

Kadhalika amesisitiza ushirikia baina ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo michezo. 

"Bonanza hili limefana sana na limenifurahisha niwapongeze sana bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maandalizi na niwasihi kuendeleza ushirikiano baina yenu na baraza la wawakilishi katika masuala mbalimbali kama hivi leo mlivyofanya katika bonanza hili,"amesema. 


Kwa upande wake Spika wa bunge La jamuhuri ya muungano wa Tanzanja Dkt Tulia Ackson amesema bajeti mpya ya serikali imegusa wananchi moja kwa moja hasa wanamichez kwa kutenga zaidi ya bilioni miambili na themanini zitakazo tekeleza mambo mbalimbali kwenye sekta hiyo ambapo amewataka wanamichezo kuendelea kumuunga mkono Rais wa jamuhur ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Naye Tuli Mwambapa ni Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja Benki ya CRDB amesema Lengo la kufanya Matamasha ni kuwakutanisha viongozi wa serikali na wananchi ambapo pia amewek wazi ujio wa CRDB Marathon ambayo itafanyika agust 18 mwaka huu.

Katika Bonanza hilo kumeshuhudiwa michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Kufukuza Kuku, kupokezana vijiti, kula, kunywa soda, kukimbia na magunia, mbio za riadha na michezo mingine.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU