UJUMBE WA THBUB WATEMBELEA GEREZA KUU LA BUTIMBA MWANZA


Namwandishi wetu,Mwanza 

UJUMBE wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ukiongozwa na Mfawidhi wa Ofisi ya THBUB tawi la Mwanza Gordian Binamungu, leo Septemba 11,2024 umetembelea Gereza Kuu la Butimba lilipo Jijini hapa.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukabidhi Redio na kuwalipia King'amuzi ikiwaa ni kutimiza ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wa THBUB Jaji Mstaafu Mathew P. M Mwaimu Julai 7, 2024 wakati alipofanya ziara ya kukagua uzingatiaji wa haki za binadamu katika Gereza hilo.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Binamungu kwa niaba ya Mwenyekiti wa THBUB Jaji Mstaafu Mwaimu.

Awali katika mkutano wa THBUB na Baraza la wafungwa na Mahabusi katika Gereza hilo, Wafungwa na Mahabusu waliiomba THBUB kuwasaidia Redio na King'amuzi ili kuwawezesha kupata taarifa kuhusu matukio mbalimbali muhimu na mambo yanayoendelea nchini hususani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kama ilivyoainishwaa katika Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

THBUB inaendelea na kazi ya kukagua sehemu walimozuiliwa pamoja na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza na kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI