MAAFISA UTUMISHI UVINZA WATAKIWA KUWAJIBIKA KWA KUIBUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI


 Na Mwandishi wetu, Kigoma  

MKUU wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Dina Mathamani amewataka maafisa utumishi wa wilaya hiyo kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao pindi wanapowatumikia wananchi kwa kuibua changamoto wanazokutana nazo katika maeneo yao.

Hayo yamejiri katika mafunzo ya Elimu ya uraia na utawala bora yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza mkoani Kigoma.

Akizungumza katika mafunzo hayo Bi.Mathamani amesema kuwa ili watumishi hao waweze kufanya shughuli zao vizuri ni lazima suala la utawala bora liweze kuzingatiwa ili wananchi wajue vitu wannavyovihitaji katika nchi yao.

Kwa upande wake Bw.Hamis Mjanja kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI amesema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kukumbusha wajibu wa kila kiongozi katika utekelezaji wa majukumu aliyopewa na serikali.

Mjanja Amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kuzingatia suala la utawala bora 

Nao baadhi ya washiriki waliohudhuria akiwemo Hedetrides na Frank Michael ambao ni watendaji wa kata wamesema mafunzo hayo wamesema mafunzo waliyopata leo watayafanyia kazi kwa kuzingatia misingi na weledi hususani katika suala la utawala bora na sheria.

Mafunzo hayo yanayoratibiwa na wizara ya katiba na sheria yameshafanyika katika mikoa mitano na kwasasa yanaendelea kufanyika katika mikoa sita na hivyo kukamilika kwake kutaongeza idadi na kufanya mikoa kumi na moja kuwa imefikiwa na mafunzo haya. 

Mikoa ambayo mafunzo hayo yanafanyika kwa sasa ni pamoja na mkoa mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro, Geita, Katavi, Tabora na Mtwara.

Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO