MAPOROMOKO YA MAJI YA MKUZI LUSHOTO YAWAKIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII


Na mwandishi wetu

WATALII zaidi ya 200 wa ndani na nje ya nchi wamefika katika Mapolomoko ya maji ya Mkuzi huko wilayani Lushoto mkoani Tanga katika mwezi Novemba Hadi mwezi Desemba mwaka huu kujionea vivutio kwa utalii katika msitu wa kituo cha utalii cha Mkusu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mhifadhi misitu wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania TFS Wilaya ya Lushoto Hassan Sengerere amesema Wilaya ya Lushoto ina Misitu 12 inayosimamiwa na kutunzwa na TFS Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga katika Halmshauri za Bumbuli na Halmshauri ya Lushoto.

Amesema Watalii hao Ili kuweza kujionea Mazingira ya misitu ya Asili iliyotunzwa ikiwamo ikiwemo mapolomoko hayo ya Mkuzi sambamba na wadudu na wanyama ikiwa ni kuungana na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amehamasisha utalii ndani na nje ya nchi.

Amesema Misitu hiyo ya Lushoto ina vivutio mbalimbali vya utalii ambapo Watalii wataweza kujionea mnyama aina ya Mbega mwenye Rangi Nyeusi na nyeupe na Mandhari ya kuvutia Utalii Katika misitu hiyo.

Hassan aliongeza kuwa pia katika maeneo hayo yanayozunguka mapolomoko ya maji ya Mkuzi kuna mimea ambayo ni adimu katika ukanda huu wa Afrka Mashariki lakini inapatikana katika uoto wa asili wa Misitu ya wilaya ya Lushoto ambayo imekuwa kivitio kikubwa kwa Watalii wa ndani na nje.

Amesema mazingira ya misitu ya kuzunguka katika mapolomoko hayo ya maji yanatunzwa kwa ushirikiano kati ya TFS na wananchi wa vijiji zaidi ya 13 vinavyozunguka Misitu hiyo ambapo pia wana kutoa elimu ya utunzaji wa Misitu ili walinde na kutunza Misitu hiyo.

"Tunatoa elimu kwa wananchi ya kuhamasisha upandaji wa miti ambayo utapunguza utegemezi wa miti katika Misitu ya wilaya ya Lushoto ili watumie mahitaji ya miti katika Misitu yao badala ya kuwategemezi kwenye Misitu ya hifadhi ya taifa" alisema Hassan 

"Lakini pia tunatoa ushirikiano katika ufugaji nyuki katika jamii zao huko huko ili kupunguza utegemezi wa msitu moja kwa Moja"" alisema 

"Pia tunatoa elimu ya kupambana na majanga ya moto ili tusaidiane kuzima moto iwapo majanga yakitokea kwenye Misitu yetu ili wasaidie kudhibiti Moyo unapotokea" alisema.

Alisema "Changamoto wanayokabiliana nayo kuwa ni pamoja na wanavijiji kuchoma mikaa na uwindaji wa wanyama aina ya digidigi kiholela ambayo hukabilisna nayo kwa kutoa elimu kwa wanavijiji hao" 

Naye George Talimo Afisa ufugaji nyuki Mwandamizi wilaya ya Handeni amesema amejionea kwa macho yake aina mbalimbali za ndege ambao ni kivutio kikubwa na wanyama aina ya Mbega wenye rangi nyeusi na nyeupe na Hali ya hewa nzuri katika maeneo ya mapolomoko hayo ya maji ya Mkuzi

Aidha Talimo ameitaka jamii kujenga tabia ya utunzaji wa mazingira ya misitu ili taifa liendelee kunufaika na vivutio vya utalii ya misitu iliyohifadhiwa vizuri hapa Nchini.

"Unapotembelea kwenye maeneo ya Utalii unanufaika kwa namna nyingi ikiwa ni pamoja na kuondoa msongo wa mawazo na kuna baadhi ya magonjwa hupona kwa kufika katika mazingira ya hifadhi ya Misitu" alisema Talimo.

Evareto Moley ambaye ni Mwalimu wa shule ya msingi Handeiyu akiwa ameongozana na walimu wenzake alisema walifika katika mapolomoko ya maji ya Mkuzi ilikujionea vivutio mbalimbali vya utalii na kufutahia Hali ya hewa nzuri ya maeneo hayo.

Pia alisema kufika katika maeneo hayo ni kuunga mkono na kuitikia jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia kuhamasisha utalii katika Nchi yetu.

Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO