WAZIRI SIMBACHAWENE:SERIKALI KUAJIRI WALIMU 14,648


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala Bora George Simbachawene ameeleza kuwa serikali imeajiri Walimu 14,648 ikiwa ni nafasi ambazo zilitolewa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa lengo la Kupunguza uhaba wa walimu nchini.

Pia ameendelea kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiriwa kwa watumishi hao.

Kauli hiyo ya serikali ameitoa leo Januari 11,2025 wakati akitoa taarifa kuhusu usaili wa kada ya ualimu unaotarajiwa kuanza tarehe 14 Januari na kumalizika tarehe 24 Februari, 2025.

Aidha,Simbachawene ameongeza kuwa usaili utafanyika katika ngazi za mikoa ili kupunguza gharama kwa waombaji ambapo amewasihi wale wote walioitwa Kwenye usahili wajiandae vyema Kwa usaili kwani nafasi ni za ushindani.

Taarifa hii inakuja wakati taifa likikabiliwa na changamoto za uhaba wa walimu, hususan katika maeneo ya vijijini, ambapo juhudi za serikali zinalenga kupunguza pengo hili kwa kuweka mikakati ya muda mrefu ya kuimarisha sekta ya elimu.

Aidha ametoa wito kwa watumishi hao ni kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, bidii na uadilifu mkubwa ili kumpa heshima inayostahili Mheshimiwa Rais kwa nafasi aliyowapa

Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO