MASHIRIKIANO YA PURA NA ALNAFT KUKUZA UBORA WA UDHIBITI WA MKONDO WA JUU WA PETROLI



Rais wa ALNAFT,  Samir Bekhti (watatu kushoto) akizungumza wakati wa kikao kati ya PURA na ALNAFT kilichofanyika Septemba 07, 2025. Wapili kulia ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Shigela Malosha



 Rais wa ALNAFT,  Samir Bekhti (kushoto) katika picha ya pamoja na mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Shigela Malosha mara baada ya kikao kati ya PURA na ALNAFT kilichofanyika Septemba 07, 2025 Jijini Algeris, Algeria.

NA MWANDISHI WETU, Algeries ,Algeria

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA) imekutana na kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli ya Nchini Algeria (ALNAFT) kwa lengo la kujadili mashirikiano yatakayowezesha, pamoja na mambo mengine, kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika eneo la udhibiti wa shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

PURA na ALNAFT zimekutana Septemba 07, 2025 Jijiji Algeries nchini Algeria katika kikao kulichohudhuriwa na Rais wa ALNAFT,  Samir Bekhti, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Bw. Shigela Malosha na baadhi ya viongozi na wataalamu kutoka pande zote.

Akizungumza katika kikao hicho,  Malosha alieleza kuwa mashirikiano baina ya taasisi hizo ni muhimu kwa ustawi wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli nchini Tanzania na Algeria kwa kuwa yatawezesha taasisi hizo kuongeza ufanisi wa shughuli za udhibiti na usimamizi wa masuala ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

"Kupitia kujengeana uwezo kwa njia ya mafunzo na kubadilishana uzoefu wa namna PURA na ALNAFT zinatekeleza majukumu, ni dhahiri kuwa mashirikiano haya yatakuwa chachu ya taasisi hizi kufanya vizuri zaidi" alisema Shigela.

Kwa upande wake, Rais wa ALNAFT alibainisha kuwa mashirikiano ya taasisi hizi ni muhimu na yatakuwa na manufaa makubwa kwa pande zote kwa kuzingangia kwamba PURA na ALNAFT zinatekeleza majukumu yanayofanana ingawa katika nchini tofauti.

Miongoni mwa maeneo ambayo PURA na ALNAFT zimejadili kubalishana uzoefu na kujengeana uwezo ni pamoja na udhibiti na usimamizi wa shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia, uhifadhi wa data za petroli, ushiriki wa kampuni za ndani katika miradi ya mafuta na gesi asilia na uandaaji wa sheria, kanuni na miongozo husika.

Post a Comment

0 Comments

SERIKALI YAHIMIZA MAADILI NA UZALENDO