WAKUU WAWILAYA WAPYA WATAKIWA KUHESHIMU VIAPO VYAO


 Na Wellu Mtaki,Dodoma

 KATIBU Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kanda ya kati Dodoma Jasmini Awadhi amewataka wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa kuheshimu na kuviishi viapo vyao walivyoviapa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa kiapo cha  Ahadi ya Uadilifu kwa Mkuu wa wilaya ya Chemba Mh Gelard Lomward Mongela  katika hafla fupi iliyofanyika  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Janauari 30,2023.

Amesema"hakikisheni mnajitoa kutumikia viapo mlivyotoa mbele yetu na kuviweka katika kumbu kumbu zenu za kila siku ili kuyakumbuka yale yote yaliyoelezwa katika viapo hivyo mnapotekeleza majukumu yenu ya kila siku"

Katika hatua nyingine  Awadhi alimpongeza Mkuu wa wilaua ya Chemba  kwa kuteuliwa kwake na alisema kuwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekupa heshima ya kubwa ya kuiongoza wilaya ya Chemba

Katibu huyo Msaidizi aliwapongeza wakuu wengine wapya wa wilaya za Bahi Mhe Godwini Gondwe na Mpwapwa Mh Sophia Kizigo waliohamishiwa mkoani Dodoma katika mabadiriko ya vituo vya wakuu wa wilaya yaliyofanyika hivi karibuni.

Hafla ya kumuapisha Mkuu wa wilaya ya Chemba na kuwakaribisha wakuu wa wilaya wapya ilifunguliwa na mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyemule ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Dodoma, Viongozi  wa dini, Viongozi wa vyama vya siasa, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na Menejimenti ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI