WIZARA YA ELIMU YAZINDUA KITUO CHA KUPOKELEA TAARIFA ZA UKATILI ,YAZUIA VITABU VISIVYO NA MAUDHUI YA KITANZANIA

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

KUTOKANA na vitende visivyo na maadili vinavyofanya na baadhi ya taasisi zilizopo chini ya Wazara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, wizara hiyo imeanda kituo cha huduma kwa wateja (Call center), ambacho kitakuwa kinapokea taarifa hizo lengo likiwa ni  kuweza kufanyiwa kazi kwa wakati.

Pia wizara hiyo imezuia Vitabu ambavyo maudhui yake hayaendani na Mila,desturi na utamaduni wa mtanzania katika shule zote zilizopo nchini.

Akizungumza jijini Dodoma katika Mji wa kiserikali leo Februari 3,2023 wakati  akizindua kituo hicho, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk.Francis Michael amesema kituo hicho kitakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni na kwamba  mtu, mtanzania yoyote atakayeona jambo ambalo sio jema  ambalo linakiuka miongozo, tamaduni na maadili  kwenye taasisi za elimu, shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo atoe taarifa kupitia namba ya mezani  0262160270 na simu ya mkononi 0737962965.

Katibu huyo amesema kuwa wanategemea kupata taarifa zinazohusu malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa taratibu na miongozo ya utoaji elimu kwa taasisi hizo za elimu na kwamba wizara hiyo imeona ni vema kuja na kituo cha kutolea taarifa zinazohusu vitendo visivyo vya maadili.

Ameongeza kuwa kama kuna mtanzania yoyote atapata taarifa za vitendo hivyo ambavyo vinaenda kinyume na maadili, miongozo na taratibu za taasisi ya elimu watumie kituo hicho.

"Kama mnavyofahamu Siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye mitandao na magazeti kumekuwa na taarifa ambazo wananchi wamekuwa wakizipata ya upotoshaji wa maadili ya watoto shuleni kwetu pamoja na tabia chafu ambazo zimekuwa zikifanya na baadhi ya taasisi zetu na tulipeleka timu na ripoti hiyo itatolewa hivi karibuni," amesema.

Ameongeza kuwa taarifa zitakazotolewa zitakuwa ni siri na kwamba mtoa taarifa hizo atalindwa kwa mujibu wa sheria.



Akizungumzia katazo la vitabu hivyo amesema kuwa Wizara hiyo katika kutekeleza wajibu wake wa kusimamia utoaji wa elimu nchini na katika kuhakikisha njia mbalimbali za ufundishaji na ufunzaji zinazingatia ubora na maslahi ya nchi, Mila desturi na utamaduni za mtanzania.

Karibu Mkuu huyo ameeleza  Wizara ilitoa waraka  namba 4 wa mwaka 2014 pamoja na sheria na nyaraka nyingine na miongozo inayohusu elimu ililenga katika kuhakikisha kuwa vitabu vya ziada na kiada vinavyotumika  katika Shule zilizosajiliwa nchini kuhakikisha vinavyotumika ninakuwa na maudhui kulingana na Mila, desturi na utamaduni wa nchi za kumlinda wa kitanzania  mtoto aliyopo shuleni.

Ameeleza kuwa katika kutekeleza wa waraka huo wizara imebani kuna baadhi ya Shule ambazo zimekuwa zikiingiza na kutumia vitabu ambavyo maudhui yake yanakinzana na mila, desturi, miongozo pamoja na tamaduni za mtanzania.

Amefafanua kuwa baadhi ya vitabu hivyo vimekuwa vikiatarisha ukuaji na kupotosha Mila na desturi za nchi katika makuzi na malezi ya watoto wa Tanzania kwa ujumla.

Aidha amewataka wamiliki wa waendeshaji wa shule za Umma na binafisi zilizosajiliwa nchini kufuata na kuzingatia waraka namba 4 vinginevyo hatua Kali zitachukuliwa pamoja na kufungiwa usajili.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI