Mbunge wa Mahonda Zanzibar Abdullah Ally MwinyiNa Asha Mwakyonde, Dodoma
MBUNGE wa Mahonda Zanzibar Abdullah Ally Mwinyi leo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kupatiwa nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Chama Cha Mapindizi (CCM),white House.
Akizungumza jijini Dodoma leo Febuari 5, mwaka huu katika Makao makuu ya chama hicho amesema anauzoefu wa miaka 10 bungeni.
"Nina furaha ya kuchukua fomu ya kukuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama changu nafasi ya Uspika,amesema mbunge huyo.
Amesema kuwa alishawahiwa kuwa mbunge wa Afrika Mashariki na kwamba tofauti ya Bunge hilo na la Tanzania ni lugha tu lile linatunia kiingereza na hilo la Tanzania linatumia lugha ya Kiswahili.
0 Comments