Mhandisi Xaday: Ninasifa ya kuomba ridhaa nafisi ya Naibu Spika

Mbunge wa Hanang' Mhandisi Samwel Xaday akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya  Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MBUNGE wa Hanang' Mhandisi Samwel Xaday leo Febuari 5, 2022, amechukua fomu ya kuwania kiti cha nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma leo Febuari 5 mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo Mhandisi Xaday amesema amechukua uamauzi huo kwa kuwa nafasi hiyo ipo wazi na sifa ya kuwania kiti hicho anayo."Nafasi hii ipo wazi baada ya aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge hilo kujiuzulu na kuchaguliwa na chama kuwa Spika nmeona sifa ya kuwa Naibu Spika ninayo," amesema.

Mhandisi Xaday ameongeza kuwa sifa ya kuwania nafasi hiyo anayo kwani tayari ni mbunge na  ana haki kwa mujibu ya Chama  Cha Mapindizi (CCM).



Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO