Mwanaharakati Bihimba Mpaya akipeana mikono na mkuuwa Shule ya sekondari Abuu Jumaa Froida Nkya
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Kivule, Kata ya kivuli iliyopo wilayani Ilalla jijini Dar es Salaam ambaye ni mwanaharakati wa masula ya kijamii yakiwemo elimu Bihimba Mpaya amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kujenga uzio wa shule ya secondari ya Abuu Jumaa.
Lengo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika uboreshaji wa Sekta ya Elimu.
Akizungumza jana shuleni hapo mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo ya saruji Mpaya amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwalinda watoto na mambo ya vishawishi ambavyo wanaweza kuvipata kutokana na mwingiliano wa watu.
Mwanaharakati huyo afafanua kuwa lengo jingine ni kukomesha utoro shuleni hapo na kuto kukaa vichakani na badala yake watakuwa ndani ya eneo la shule na kujisomea.
Pia mwanaharakati huyo amewataka wadau wengine kujitokeza kuweza kusaidia shule hiyo ili iweze kukamilisha uzio huo.
Kwa upand mkuu wa shule Abuu Jumaa Froida Nkya amesema wanamshukuru Mpaya kwani ni miongoni mwa wadau muhimu wa elimu.
Amesema katika shule hiyo mdau huyo amekuwa ni chachu katika masula mabalimbali ikiwamo ya kukamilisha ukuta wa shule kwa kutoa kwa mara nyingine tena saruji ili kuhakikisha ukuta unakamilika.
"Ukuta utakapo kamilika utasaidia kuzuia utoro wa wanafunzi hatimae kuzidi kuinua ufaulu wa wanafunzi katika shule hii,"amesema Mkuu huyo wa shule mwalimu Nkya.
0 Comments