Dkt.Gwajima:Mashirika yasiyo ya kiserikali 6,147 yanatekeleza majulumu yake kati ya 11946 yaliyosajiliwa

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum  mhe.Dkt. Dorothy Gwajima akisoma taarifa ya usimamizi wa  maahirika yasiyo ya kiserikaliN

NA WMJJWM, DODOMA

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amebainisha kuwa, jumla ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 6,147 ndiyo yanatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni kati ya Mashirika 11,946 yaliyosajiliwa mwaka 2005 hadi Januari, 2022.

Mhe.Dkt. Gwajima amebainisha hayo wakati  akitoa taarifa ya usimamizi, utekelezaji, mafanikio na changamoto za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa kipindi cha 2019/2021 mbele ya  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Aloyce Kamamba, amesema hakuna sababu ya kuwa na orodha kubwa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati yanayofanya kazi kwa mujibu wa sheria ni Mashirika machache.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wamepongeza jitihada zinazofanywa na Wizara katika kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa NGOs na kusisitiza kuboresha mikakati iliyopo. 

Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO