UDOM YAPONGEZWA KUSHIRIKI MAONESHO WIKI YA SHERIA, KURAHISISHA MICHAKATO WA HAKI

Na Asha Mwakyonde,DODOMA

CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kupitia Shule Kuu ya Sheria kinapaswa kuigwa na Vyuo vingine vyote ambavyo bado havijapata fursa ya kuanza kushirikiana na taasisi nyingine katika maonesho mbalimbali kutoa elimu ya kisheria.

Hayo ameyasema Januari 28,2025 jijini Dodoma na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu yaTanzania, Dk.Mustapher Siyani alipotembelea banda UDOM katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kufanyika Kitaifa Viwanja vya Nyerere ‘Square’ amesema ushiriki wa shule hiyo ni kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Ameeleza kuwa ni jambo kubwa kila taasisi yenye shule ya kutoa msaada ni vizuri kuunga mkono jitihada za Serikali.

Jaji Kiongozi huyo amesema kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan angekuwa akionesha mwelekeo wake ni kuhakikisha wananchi wengine wanapata mwanga katika eneo zima la haki.

"Nimekuja kwenye banda hili nikiwa sina swali lolote lakini nimekuja kuwapongeza kwa sababu sio vyuo vyote vinatenga nafasi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ," ameeleza.

Aidha ameongeza kuwa amefurahi kuona wananchi wa Dodoma wamejitokeza kwa wingi siku chache ambazo shule hiyo ipo katika maonesho hayo huku akisema hakutarajia kuona idadi kubwa ya watu waliofika kutembelea banda hilo.

"Nimepita hapa kuwapongeza kwa kazi mnayoifanya ya kutoa elimu ya kisheria hivyo vyuo vingine vijitokeze kwakuwa nao ni wataalam, utaalam usiishie kufundisha wataalam katika fani mbalimbali zinapotokea fursa waje kuwaelimisha wananchi," amesema.

Awali Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Rashid Ibrahim amesema kuwa Shule hiyo inatoa elimu ya sheria ikiwamo shahada ya Sheria ya kwanza, uzamili na Uzamivu.

"Shule hii pamoja na kutoa elimu ya sheria, UDOM ina kituo cha msaada wa kisheria ambacho kimasajiliwa kama Kituo cha kutoa msaada kisheria,

Mhadhiri huyu ameeleza kuwa uwepo wao kwenye maonesho hayo wameweza kuhudumia watu wenye changamoto mbalimbali za kisheria yakiwamo masuala ya ardhi na mirathi.

Post a Comment

0 Comments

TAARIFA ZA WASTAAFU NHIF KUHAKIKIWA MAHALI WALIPO