Na Asha Mwakyonde, DODOMA
KATIKA suala la haki Jinai Mamlaka ya Mabaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), inasaidia mahakama kutoa uamuzi kwenye mashauri mbalimbali.
Hayo ameyasema Januari 28 jijini Dodoma na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk.Mustapher Siyani alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea kufanyika Kitaifa Viwanja vya Nyerere ‘Square’ amesema kwa sasa kila mwananchi anaamini taarifa zinazotoka katika maabara hiyo hazijachakachuliwa.
"Uwepo wenu kila wakati kwenye haya maonesho inaonesha ni jinsi gani maabara hii imejipanga kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu kazi za mamlaka," ameeleza Jiji Kiongozi Dk.Siyani.
Awali akitoa maelezo mafupi kuhusu baadhi ya mifumo inayotumiwa na mamlaka hiyo Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai kutoka GCLA, David Elias amesema kuwa Mfumo wa Usimamizi wa Taifa za maabara (LIMS), unafanya kazi namna unavyofanya kazi katika taasisi za Serikali kwa kutoa ushahidi.
Amesema lengo la mfumo huo ni kutoa matokeo kwa wakati ili waweze kufungua kesi mahakamani na kupunguza msongamano wa mahabusu gerezani.
"Kitu ambacho kimeongezwa na serikali kupitia maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni Ithibati ya maabara ambapo matokeo yanayotoka yana Ithibati ambayo inatambukika kitaifa na kimataifa," amesema.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa makosa ya Jinai hayana mipaka ndio sababu ya kuongeza Ithibati hiyo hivyo matokeo yanayotoka yawe na sifa za kitaifa na kimataifa.
0 Comments