Na Asha Mwakyonde, DODOMA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajia kuwatambulisha Viongozi wake kwa wanachama wa Chama hicho walioteuliwa katika mkutano Mkuu uliofanyika hivi karibuni jijini Dodoma kwenye sherehe za miaka 48 ya CCM.
Viongozi hao ni Rais Dk Samia Suluhu Hassan mgombea nafasi ya urais Tanzania Bara, mgombea Mwenza wa kiti cha Urais Dk. Emmanuel Nchimbi na mgombea Urais Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi.
Hayo yamesemwa leo Februari 3, 2025 jijini Dodoma na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM),CPA Amos Makalla wakati akizungumzia maadalizi ya sherehe hizo amesema kuwa maadalizi ya sherehe hizo yanaendelea vizuri kama ambavyo wamefanya katika mkutano Mkuu wa Chama hicho uliofanyika hivi karibuni.
"Pamoja na matukio mengine yote kuna tukio jingine tumeliongeza la kuwatambukusha wagombea wetu ambao waliteuliwa katika mkutano Mkuu Rais Dk Samia, Dk.Nchimbi na Rais wa Zanzibar tutawatanbulisha wagombea wetu kwa wanachama wa CCM," ameeleza.
Ameongeza kuwa muda utakapofika watawatambulisha kwa wananchi huku akisema tukio hilo ni la kipekee na kwamba CCM kinatimiza miaka 48, kikiwa imara ambapo kina wanachama zaidi ya milioni 12.
Makalla amesema kuwa Chama hicho kina wamachama wengi kuliko Chama kingine hapa nchini ambacho kinatekeleza Ilani yake.
"Chama kinafikisha miaka 48 kikiwa na wanachama zaidi ya zaidi ya milioni 12, na katika uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania Bara kilipata ushindi asilimia 98," ameema Katibu huyo.
Pia amewashukuru viongozi wa Chama hicho wa mikoa yote kufanya vizuri sherehe hizo na mbazo zinatarajiwa kuhitimishwa Februari 5, mwaka huu.
Aidha CPA Makalla amewataka wananchi wa Dodoma na wa mikoa ya jirani kuhudhuria kwa wengi kwa kuwa sherehe hizo sio mkutano hazina kadi.
0 Comments