DC KONGWA AIPIGIA MWINGI YOUNG C.E O'S WOMEN


Naibu waziri Ofisi ya waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga ( Kati Kati), kwa upande wake wa Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi wa kampuni ya Shule yetu Helena Kalolo, na (kushoto) kwake ni Mwandaaji wa Young C.E.O'S Women Anna Kimpa na Mwanasaikolojia Gloria Kasiro.

Na Asha Nwakyonde, Dodoma

MKUU wa Wilaya ya Kongwa Remidius Mwema amesema kuwa wataiangalia kampuni ya ZE Future Company Limited Present (Young C.E.O'S Women),kwa sura ya kitaifa na kimaifa kwa kuiunganisha  na wajasiriamali wakubwa kimasoko.

Mwema ameyasema hayo jana jijini hapa  wakati akifungua jukwaa la wajasiriamali wadogo wakike wa Mkoa wa Dodoma lengo likiwa ni kuanzimisha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya kazi kubwa ya kuiongoza nchini na kuendeleza vema miradi mikubwa katika sekta mbalimbali pamoja na kuupiga mwingi katika mataifa mengine.

Amesema wajasiriamali hao wametiwa moyo na kiongozi wa nchi Rais Samia kwa kuwa amewawekea mazingira rafiki ya kufanyia biashara na kwamba hata wafanyabishara wadogo wadogo (Machinga), kwa Mkoa wa Dodoma tayari ujenzi wa soko la kisasa umeshaanza.

Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kuwa Rais Samia ni kiongozi ambaye amekuwa ni kielelezo kwa watu wote wa Tanzania na kwamba hata Young C.E.O'S Women nao wametambua mchango wa Rais na  kumpongeza.

" Nimepata mwaliko wa Ze Future Company Limited Present  (Young C.E.O'S Women), ambao ni wjasiriamali wa Mkoa wa Dodoma, ni Vijana wadogo wakike wameamua kuunganisha nguvu ya pamoja  hii imefanyika kwa mara ya kwanza na kilichonifurahisha ni namna walivyokutana," amesema.

Amesema kuwa wajasiriamali hao wa Young C E.O'S wamekutana kupitia mitandao ya kijamii hasa WhatsApp ambapo walikutana na kufahamiana na kwamba kwa kipindi kirefu wamekuwa wakikutana kusaidia jamii yanye uhitaji kwa kile kidogo walichokuwa nacho wanachangisha.

Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kuwa jukwaa hilo ni la msingi kwa kuwa wanafahamiana na kubadilishana mawazo, uzoefu na kukabiliana na changamoto mbalimbali za shughuli zao za ujasiriamali kutokana na baadhi yao kufanya shughuli hizo za aina tofauti toafuti.

"Mimi kama kiongozi wa serikali nimefurahishwa na jambo hili ambalo ni jema tutaendelea kuwa walezi na kuwashauri na kuwaunganisha na wajasiriamali wakubwa wa Mkoa na Watanzania kwa ujumla lengo lake ni waweze kupanua wigo,"ameeleza Mkuu huyo wa Wilaya.

Mwema amefafanua kuwa wataiangalia  kampuni ya Young C E O'S Women waliyonayo wajasiriamali hao kwa sura ya kitaifa na kimataifa kwa kuwaunganisha  na wajasiriamali wakubwa ndani  na nje ya nchi kimasoko na kuwatengenezea njia ya kupata bidhaa zao hata katika mataifa mingine.

" Natoa wito kwa wajasiriamali mali wa mikoa mengine waweze kuiga hiki kinachofanyika . Miongoni mwa waanzilishi wa kampuni hii baadhi yao nafahamu historia zao walipotoka, hivyo kuna ushuhuda ambao wengine wakiweza kusikiliza inaweza ikawatia moyo," amesema.

Amefafanua kuwa kufanikiwa sio jambo la siku moja Kuna wengine wamepiga hatua kupitia jukwaaa hilo wanakumbushana walipotoka.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa amesema ujasiriamali haumzuii mtu kufanya kazi  mtu anaweza kuwa ni daktari, mwanahabari, lakini akawa mjasiriamali.

Ameeleza kuwa wajasiriamali hao wa kike wamekuwa chachu kwa Vijana wa kiume kwani hakuna jukwaa la Vijana wa kiume na wakafanya kama walivyofanya Young C.E.O'S Women.

Naye Mwandaaji wa jukwaa hilo la Young C E.O'S Women, Anna Kimpa amesema  kuwa kutokanana na juhudi za Rais Samia katika utendaji kazi  wake wameona wao kama wajasiriamali wenye kampuni hiyo  waanzimishe mwaka mmoja wa Rais huyo kwa kuwaunganisha wajasiriamali hao.

Amesema Rais Samia anastahili kuungwana mkono katika uongozi wake kwani amekuwa ni chachu kwa wanawake wa ndani ya Tanzania na nje ya nchi.

"Rais Samia anatupa moyo kwa namna anavyoiongoza nchi vema na utendaji kazi wake unaridhisha ndio maana sisi wanaweke tunapata nguvu ya kufanya shughuli zetu  kwa kuwa tunamuangalia kama kioo katika mafanikio yetu," amesema Kimpa.

Ameongeza kuwa jukwaa hilo linawakutanisha wajasiriamali wa  kike ambao  wanabadilishana mawazo, uzoefu pamoja na kujitangaza kimasoko katika biashara zao.

Post a Comment

0 Comments

TUENDELEE KUOMBA MUNGU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA MPOX