Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema Katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan imetoa sh.bilion 19 ambazo zitakazotumika kukarabati miundombinu ya kisasa ya michezo katika shule 56 nchini lengo kuibua vipaji.
Pia kwa upande wa utamaduni katika kipindi Cha mwaka mmoja shirika la Umoja wa Mataifa la Sanyansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), limeidhinisha lugha ya kiswahili kuwa na siku yake Duniani ambayo inaazimishwa Kila mwaka Julai 7.
Aidha imesema tayari imekamilisha usanifu wa ujenzi wa uwanja Dodoma ambapo unaweza kuanza wakati wowote.
Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mohammed Mchengerwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwaka mmoja akiwa madarakani amesema tayari wizara imekamilisha usanifu ujenzi wa uwanja wa Dodoma ambayo utarijiwa kuanza kuanzia Sasa.
“Ukarabati wa shule hizi 56 nchi nzima utasaidia kulea vipaji mbalimbali vya michezo kwa wanafunzi hiyo itasaidia kuibua vipaji vipya vya wanafunzi,”amesema
Mchengerwa amesema pia serikali imetenga sh.bilion 1.3 kwaajili ya kujenga kituo chaumahili katika michezo ambacho kitajumuisha viwanja,ofisi na mabweni katika chuo cha maendeleo ya michezo.
Waziri huyo amesema hadi kufikia Februari mwaka huu kiasi cha sh.bilioni 1.55 zimepokelewa kutoka Hazina ambazo zimeweza kusaidia kuendeleza maendeleo mbalimbali ya michezo nchini.
Waziri huyo ameeleza hadi kufikia Februari mwaka huu kiasi cha shilingi bilioni 1.55 zimepokelewa kutoka Hazina ambapo zimeweza kusaidia kuendeleza maendeleo mbalimbali ya michezo na zitasaidia programu za uendelezaji wa miundombinu.
“Katika kipindi cha mwaka mmoja Serikali imeanza kufanyia kazi tatizo kubwa la ufadhili katika michezo ambapo amedai huko nyuma timu za Taifa zilikuwa zikipata shida zinaposhiriki mashindano ya Kimataifa,”ameongeza.
“Mheshimiwa Rais hakuishia hapo akaridhia Serikali yake katika kipindi hichi kuanzia Julai mosi 2021 iliridhia asilimia 5 ya kodi inayokusanywa kupitia michezo ya kubashiri matokeo (Sport Betting) kutumika kuendeleza michezo nchini,”ameeleza.
Mchengerwa amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kujenga kituo cha umahiri katika michezo ambacho kitajumuisha viwanja,ofisi na mabweni katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.
Katika sekta ya Sanaa ,Waziri Mchengerwa amebainisha kuwa ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia imefanikiwa,kuanzisha mifumo ya kidigital kuwahudumia wadau wa Sanaa,kuanzisha tuzo za filamu nchini na muziki,kuongezeka kwa makusanyo na kutolewa kwa mirahaba.
Pia, amefafanua Wizara imefanikiwa kuongeza usajili wa kazi za Sanaa,kuratibu mashindano ya urembo na mitindo kwa viziwi Tanzania.
“Hadi Disemba 31 mwaka jana sh.milion 312.2 zilikusanywa na kugawanywa ambapo kazi za Sanaa 5924 zilifuzu vigezo vya kupata mirabaha ambapo jumla ya wasanii 1123 walinufaika na mirabaha hiyo,”amesema.
0 Comments