WALIOKAMILISHA DOZI YA UVIKO-19 KUINGIA, KUTOKA NCHINI BILA CHETI CHA CHANJO


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  akizungumza jijini hapa wakati akitoa ripoti ya hali ya ugonjwa wa UVIKO-19 tangu kuingia nchini machi 16 mwaka 2020 kwa kipindi cha miaka miwili sasa.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imesema kuanzia kesho Machi 17, 2022, imewaondolewa wasafri  hitaji la kuwa na cheti cha kipimo cha kuthibitisha kutokuwa na maambukizi (Negative RT PCR Certificate kilichokuwa kunahitajika  hapo awali.

Pia imesema kuwa Huduma ya Kipimo cha haraka (Covid 19 Rapid Antigen Test),zitaanza kutolewa ndani ya wiki moja katika vituo mbalimbali vya huduma za afya nchini.

Akizungumza jijini hapa wakati akitoa ripoti ya hali ya ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kipindi cha miaka miwili tangu ugonjwa huo uingie nchini, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali imelegeza  masharti hayo kwa wasafri wanaoingia  na kutoka nchini ambao wamekamilisha dozi  ya chanjo ya UVIKO-19.

Waziri Ummy amefafanua kuwa masharti hayo na mengine yataainishwa kwenye miongozo wa wasafri ambao utakuwa ukibadilika kulingana na mwenendo wa maambukizi ya ugonjwa huo nchini na Duniani kote kwa ujumla.

" Kwa kuzingatia hali ya sasa maambukizi ya UVIKO-19  nchini na mwenendo wa ugonjwa huo nchini bado upo katika  nchi yetu," amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa serikali kupitia Wizara hiyo itaendeleza mikakati mbalimbali ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19 ikiwamo kuimarisha ufuatiliaji wa hali ya ugonjwa huo ndani na nje ya nchi  na kushirikisha jamii  katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Pia amesema kuimarisha huduma za ukaguzi wa afya kwa wasafri wabaoingia katika maeneo ya viwanja vya ndege, Bandari  na mikapa ya nchi kavu.

Waziri Ummy akizungumzia hali ya UVIKO-19 tangu kuingia nchini machi 16, mwaka 2020 amesema hadi kufikia Machi 15 mwaka huu jumla ya watu 33,789 wamethibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo  na watu 803 wamepoteza maisha nchini.

Aidha amesema serikali inaendeleza kuikinga jamii kwa kuwezesha upatikanaji wa chanjo  ya UVIKO-19 ambapo hadi kufikia Machi 12, mwaka huu jumla ya watu 2, 820, 545 wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea  wanepata chanjo  kamili dhidi ya ugonjwa huo.



Post a Comment

0 Comments

TUENDELEE KUOMBA MUNGU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA MPOX