WAZIRI TAX ATAJA MAFANIKIO TISA MUHIMU KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena Tax wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja kipindi cha serikali ya awamu ya sita jijini Dodoma.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa la limetaja mafanikio Tisa yakiwamo kulipa madeni ya Wazabuni waliotoa huduma mbalimbali yenye kiasi cha shilingi bilioni 175.

Hayo yameelezwa leo  Machi 15,2022, jijini Dodoma na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena  Tax wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja kipindi cha serikali ya awamu ya sita amesema serikali kupitia Wizara hiyo imeweza kulipa wananchi fidia.

FIDIA

Amesema kiasi cha shilingi bilioni 8.015 kimetolewa na serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi katika maeneo ya Chato, kiboya (21KJ), Kikombo Dodoma, Mitwero Lindi, Nyabange Butiama na mashindo Lindi.

Aidha amesema uthamini na uhakiki umekamilika katika Maeneo ya Chato, Kaboya (21KJ), Kikombo Dodoma, Mitwero Lindi, Nyabange Butiama,na Ras Mishindo Lindi.

Aidha amesema uthamini na uhakiki umekamilika katika Maeneo ya Ras Nondwa Kigoma, Nyagungulu Mwanza, Nyamisangura Tarime, Usule Tabora na Duluti Arusha wenye kiasi cha zaidi bilioni 10.

ULINZI

Waziri huyo amesema  katika serikali ya awamu ya sita Rais  Samia  Suluhu Hassan amehakikisha kuwa nchi ipo salama

Amesema Wizara hiyo imepata mafanikio mengi ikiwamo ya kujengewa asilimia 80 kwa ajili ya matumizi  imetengewa katika Wizara ya ulinzi na kwamba kiasi kilichosalia kinatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka wa fedha.

"Kama tunavyo fahamu jukumu la Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ni kulinda Jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania dhidi ya maadui kutoka ndani na nje ya nchi na kuhakikisha mamlaka, maslahi mapana ya nchi yetu yanakuwa salama," amesema.

Waziri huyo ameongeza kuwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Wizara ya Ulinzi na JKT  kupitia Jeshi la wananchi (JWTZ), imeendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi na imeendelea kuwa shwari.

Amefafanua kuwa kumekuwapo na changamoto  chache katika baadhi ya mipaka hususani mpaka wa kusini  na kwamba changamoto hizo zimetatuliwa ipasavyo na hali ya amani na utulivu imeendelea kutamalaki.

MIGOGORO YA ARDHI

Dk. Tax amesema Wizara ya Ulinzi na JWTZ chini ya Rais wa awamu  ya sita imeweza kushughulika migogoro ya Ardhiipatayo 74 huko Arusha Chukwani, Dar es Salaam, Dodoma,Kagera, Kigoma, Lindi,Mara, Morogoro, Mwanza, Njombe,Pwani,Rukwa, Ruvuma,Shinyanga, Singida,Tabora,na maeneo ya Kisakasaka huko Zanzibar.

"Zoezi hili linaendelea kwa maeneo ya Walezo, Buvuai, Ubago,Dunga,na Unguja Ukuu huko Zanzibar hadi Sasa jumla ya shilingi bilioni 8.015 kimetolewa na serikali ya wamu ya sita kwa ajili ya kuwalipa fidia," amesema waziri huyo.
 
Ameongeza kuwa uthamini na uhakiki umekamilika katika maeneo ya Ras Nondwa Kigoma, Nyagungulu Mwanza, NyamisangurTarime,Usule Tabora, na Duluti Arusha wenye kiasi cha zaidi ya  bilioni 10.

Dk.Tax ameeleza kuwa maaeneo 50 tayari yameshafanyiwa upimaji na utathimini na utathimini huo ambao haujaisha ni wa mpakani  na kwamba uhakiki unaendeleaje.

KUPANDISHA WATUMISHI VYEO 

Amesema kuwa Wizara chini ya serikali ya awamu ya sita imeweza kuwapandisha vyeo watumishi 74 na kuendelea kutoa mafunzo.

Waziri huyo ameongeza kuwa umahiri wa wanajeshi unategemea mafunzo yanayohitajika katika kipindi cha mwaka mmoja na kwamba jeshi la JWTZ  limewezeshwa kutoa mafunzo ya kijeshi katika shule na vyuo vya kijeshi  ndani na nje ya nchi.

MAZINGIRA YA UTENDAJI KAZI

Amesema serikali imeendelea kudumisha uhusiano wa kimataifa na kitaifa katika dekta ya Ulinzi hususani kushirikiana na Umoja wa Kimataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU),  na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), katika Operesheni mbalimbali za Ulinzi wa amani kwa kupeleka vikosi na usaidizi, waangalizi wa jeshi, wanadhimu na makamanda nchi zenye migogoro.

AJIRA

Waziri Tax amesema pamoja na taasisi zilizopo chini yake imefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 9341 kupitia miradi mbalimbali za kudumu  na za muda mfupi.

Amesema serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika uendelezaji wa miradi ya kielelezo  na kimkakati kwenye Wizara hiyo kupitia JWTZ.

Pia serikali imeendelea kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa baadhi ya miradi hiyo ikiwamo  Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR).

AFYA

Dk.Tax amesema kwa kutambua umuhimu wa afya bora kwa wanajeshi na wananchi Wizara kupita JWTZ na JKT imeendelea kutoa huduma za matibabu kwa maafisa, Askari, Vijana wa jeshi la Kujenga Taifa, watumishi wa Umma na familia zao pamoja na wananchi wanaoishi karibu na vituo vya tiba vya jeshi hapa nchini.

" Wizara kupitia JWTZ inandelea na ujenzi wa Hospitali ya jeshi  maeneo ya Msalato jijini hapa kwa kushirikiana na serikali ya Ujerumani  ambapo ilitoa bilioni 20.

TEKNOLOJIA

Amefafanua kuwa Wizara kupitia mwashirika yake ya Tanzania Automotive teknology Centre (TATC) na MZinga imeendelea kufanya utafiti na uhawilishaji wa teknology kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na huduma mbalimbali kwa matumizi ya kijeshi na kiraia.

Dk. Tax amesema serikali ya awamu ya sita imetoa kipaumbele kwa kutoa rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango  wa miaka 10 wa kuliimarisha shirikaka  ili liweze kutekeleza majulumu yake kwa ufanisi.

KUPAMBANA NA UVIKO-19

Amesema serikali hiyo kupitia Jeshi hilo limefanikiwa kutekeleza na kusimamia mikakati ya Kupambana na ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO-19), kwa kutoa elimu ya kujikinga  na kuelimisha kuhusu umuhimu wa chanjo.

Pia amesema jeshi limepambana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi kwa kutoa elinuya kujikinga ili kuzuia maambukizi mapya na kupubguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.

" Mafanikio haya ambayo Wizara imayapata katika kutekeleza majukumu yake na uwezo wa Wizara na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania unatoka na serikali ya awamu ya sita,"ameeleza.

Aidha amempongeza Rais Samia kwa jinsi ambavyo ameweza kulivusha Taifa na kuiongoza nchi kwa umahiri.

Post a Comment

0 Comments

TUENDELEE KUOMBA MUNGU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA MPOX