MSHUI:WANAWAKE TUMUUNGE MKONO RAIS SAMIA KATIKA JITIHADA ZAKE

Wanawake wa Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu, Chemba

WANAWAKE wametakiwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa  anayofanya inayodhihirisha wanawake wakiwa viongozi wanaweza kufanya makubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Wakuzingumza wakati wa mahojiano hivi karibuni  kwenye maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika katika Mkoa katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma walisema wataendelea kumuunga mkono Raisi Samia kutokana na.jitihada kubwa anazofanya kwenye uongozi wake katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Mwenyekiti wa wanawake Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Dodoma Fatuma   Mshui alisema 
Maadhimisho ya mwaka huu yamefana sana zikiwa ni juhudi za kuonesha kuwa wanawake wanaweza na wapo pamoja na Rais Samia.

"Sisi   kama wanawake tumejitokeza sana Ili kumpa sapoti Rais Samia kwa kuwa anafanya kazi kubwa sana na kazi anaiweza,  kama wanawake tupo nyuma yake  kutoa sapoti , Rais Samia anaupiga mwingi, lazima tumuunge mkono kwani sisi ni Jeshi kubwa" alisema
Alisema juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita zinatakiwa kuungwa mkono na wananchi  wote.

Ezita Kadwela ambaye pia ni Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Dodoma alisema uelekeo unaonesha wanawake wanaweza na wanatafuta usawa wa 50 kwa 50 

"Maadhimisho ya mwaka huu yamekuwa mazuri kwa sababu ya Raisi wetu ni mwanamke na wanawake watafanya makubwa kama Raisi anayovyofanya,  sisi wanawake tunaweza kuongoza na kufanya mambo makubwa," alisema.

Mkazi wa Mrijo Weilayani Chemba Amina Juma alisema juhudi kubwa zimefanywa na Rais na wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono na hata kumuombea kwa Mwenyezi  Mungu Ili afanye mambo makubwa zaidi.

" Kwenye suala la ujenzi wa madarasa lazima tumpongeze Rais Samia kwani miaka ya nyuma kulikuwa na michango kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa lakini mwaka jana Serikali ilitoa fedha nyingi kwa ajili ya Ujenzi huo," alisema.

Pia aliwakaka wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngaci za vijiji Ili idadi ya wanawake viongozi iongezeke.

Aidha Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa maadhimisho  hayo mmoja wa wanawake waliofanikiwa Juliana Assey ambaye ni mmlili wa Shule ya Alshaday alisema tangu akiwa binti mdogo alikuwa na ndoto ya kumiliki.shule.

" Nilikuwa na ndoto za kuwa na Shule yangu, lakini nilipowaekeza watu wangu wa karibu walisema  ninaota ndoto ambazo hazitekelezeki,sikukata tamaa nikamtafuta Mchungaji Getrude Rwakatale ( Marehemu) ambaye wakati huo alikuwa na shule, haikuwa kazi rahisi kumpata lakini nilipata bahati ya kukutana nae nikamueleza ndoto yangu akaniambia  wazo lako, ndoto yako ndiyo Shule yenyewe hakuna lisilowezekana," alisema.

Alisema baada ya hapo alifanya jitihada mbalimbali na kwa miaka 16 alikuwa akihangaika kufuatua matofali na kutafuta fedha za mafundi na kuanza kupandisha vyumba.vya madarasa.

"Ile Shule ilianza na mtaji wa Sh 100,000 aliyonipa mama Rwakatale siku nilipoenda kumsalimia na fedha ile ilikuwa kama ya Baraka kwani nilizotumia kuanza kufuatia matofali na kuendelea kidogo kidogo kwa kutumia kipato changu,' alisema.
Aliwataka wanawake kutokana tamaa na kuzifanyia kaci ndoto zao.

Post a Comment

0 Comments

TUENDELEE KUOMBA MUNGU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA MPOX