Imamu wa Msikiti wa Al Masjid Nuur Islamiya (kushoto),Ustazi Hussein Udenda (Kulia), Mwanaharakati Huru Bihimba Mpaya wakipeana mikono ishara ya kukabidhiana mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Al Madrasat.
Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
MWANAHARAKATI Huru wa masuala ya kijamii, Mkazi wa Kata ya Kivule iliyopo Wilaya ya Ilala jijni hapa Bihimba Mpaya ametoa msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Madrasa iliyopo chini ya msikiti wa Al Masjid Nuur Islamiya.
Akizungumza jijini hapo mara baada ya kukabidhi msaada huo Mpaya amesema mifuko hiyo kwa ajili ya ujenzi wa Madrasa ya Al Madrasat Nuur lengo likiwa watoto wa kiislamu wape elimu ya dini.
Mwanahabari huyo amesema ametoa mifuko hiyo baada ya kusikia kiongozi wa masikiti huo akiomba wafadhili kuchangia ujenzi ndipo akaguswa kuchangia ujenzi wa Al Madrasat hiyo.
" Nimeguswa kama kijana muumini wa kiislamu nilisema muda ukifika siku ya Ijumaa nitaleta sadaka yangu ya mifuko ya saruji na leo Mwenyezi Mungu amenijaalia uzima na afya nimeweza kuleta," amesema Mpaya.
Aidha Mpaya ameiomba jamii, taasisi na serikali kusaidia ujenzi wa Madrasat hiyo.
Akipokea msaada huo Imamu wa msikiti wa Al Masjid Nuur, Ustazi Hussein Udenda amemshukuru Mpaya kwa msaada wa mifuko ya saruji ambayo inaendeleza ujenzi wa Madrasat hiyo.
"Mpaya ametoa alichojaaliwa nacho tunamuombea afya njema na Mwenyezi Mungu amjaalie moyo huu wa kutoa na aendelee kutoa zaidi na zaidi," amesema Ustazi Udenda.
Awali Sheikh wa msikiti huo Hussein Lugome ameeleza kuwa mifuko hiyo ya saruji imefika siku nzito ya Ijumaa na kwamba Mpaya amekabidhi baada ya swala ya Ijumaa.
0 Comments