CHONGOLO AWAONYA MAKATIBU CCM



Katibu Mkuu wa Chama Cha Cha Mapindizi, Daniel Chongolo akizungumza  wakati alipokuwa akifungua kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Juni 15, 2022 jijini Dodoma.

Na Asha Mwakyonde Dodoma

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema bajeti ya ya mwaka wa fedha 2022/2023 imejiielekeza kwenye maeneo ya msingi na imebeba matumaini ya Watanzania hasa Wanawake  kwa serikali yao pamoja na kubeba mwendelezo wa kasi ya kujenga  kiuchumi wa nchi hasa 


Pia ametoa onyo kwa Makatibu wa CCM na Jumuiya zake kuacha mara moja kupanga safu za uongozi kabla ya muda kufika na kwamba kiongozi bora ni yule anayejiamini.

Hayo ameyasema Juni 15, 2022Jijini hapa wakati alipokuwa akifungua kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), amesema  taarifa  za kuwa Makatibu wa chama hicho  na jumuiya wanazungushwa kutoka hotel moja kwenda nyingine na kusahau kuwa wao ni wakurugenzi wa uchaguzi anazo.

"Makatibu wangu mnajiingiza kwenye ushabiki wa kutafuta na kutengeneza wagombea endapo ukibainika utakuwa umwpoteza kazi na hao wanaowazungusha hawataweza kuwasaidia pindi mtakapo poteza kazi zenu, kazi mbaya ukiwa nayo na ni nzuri kama huna waaulizezwni ambao walikuwa na kazi baadae wakapoteza," amesema.

Amesema Makatibu wa chama na Jumuiya waache kubebana bebana kwenye hoteli moja kwenda nyingine kwa kufanya hivyo ni kutia aicha na kukirudisha nyuma chama.

 Katibu huyo ameongeza kuwa kuna watu wameshajitengenezea wagombea kwa nafasi mbalimbali bila kukumbuka kama kuna viongozi waliopewa dhamana, katiba kanuni na miongozo halali ya chama.

"Tunataka mtu au kiongozi akisimama Watu waseme mwenye Jumuiya yake amesimama hii ni Jumuiya mama hatutaki Viongozi  ambao ni mabingwa wa kukopi sifa za wenzao," ameeleza Chongolo.

Amefafanua kuwa  mtu kutangaza nia wakati ukifika sio dhambi wala kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi sio dhambi ila kuna mambo yanayotaka kujitokeza hayafurahishi kwani watu wako busy tayari wameshajipatia nafasi.

"Mbaya zaidi ni pale tunapoona viongozi wakubwa wameshapewa wagombea Mimi taarifa huwa napewa taarifa juu ya chama chetu na kile kinachoendelea ndani ya chama hivyo ni aibu kuona mtu mzima anatumia jina la kiongozi wake kuwa anatumika na  kiongozi wake achukue fomu na kugombea nafasi fulani.

Na kuongeza Kusema "Kiongozi anayedhamiria kuwa kiongozi na anayejiamini haitaji kutumia jina la mwingine ili afanikiwe bali kiongozi anayejiamini anajipima nafasi yake ajithamini vigezo na sifa Ni za kwake na sio sifa za mwingine," amesema .

Awali akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka amesema chaguzi za matawi zimepita salama na wanawake wameonekana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali huku akisema chaguzi za matawi zimetoa picha chaguzi zimekwenda vizuri .

Naye Naibu Katibu Mkuu Bara Christina  Mndeme amewataka wanawake kuonesha kwa vitendo kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia unaoonekana kushika kasi kwani Jumuiya yetu inahusika katika kuhakikisha tunapinga vikali vitendo hivvyo.





Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU