MKAKATI WA UTOAJI WA HUDUMA WA AFYA YA AKILI WAJA







a. Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Tiba Dkt. Omary ubuguyu wakati wa mahojiano na Televisheni ya Channel Ten wakati wa kipindi cha baragumu mapema wiki hii.

Na Catherine Sungura,WAF-Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya afya inatarajia kukamilisha mkakati wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa  afya ya akili  ikiwemo afya ya akili mashuleni,kazini pamoja na kwenye jamii.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Tiba Dkt. Omary ubuguyu wakati wa mahojiano na Televisheni ya Channel Ten wakati wa kipindi cha baragumu mapema wiki hii.

Dkt. ubuguyu alisema mkakati huo unatarajia kutoka mwaka huu ambapo utajikita katika sehemu tatu ikiwemo afya ya akili mashuleni na kutaja kuwa  sehemu kubwa ambayo watu wanaweza kupata shida na magonjwa mengi ya afya ya matatizo ya akili  yanatokea kabla ya miaka 25.“Aidha, changamoto kubwa zitatokea hapo  chini au wagonjwa wengi wataonekana kwenye umri huo”.

Kwa sehemu ya afya ya akili makazini Dkt. Ubuguyu alisema sehemu hiyo ndio inayoathiri kwa  kiwango kikubwa  kuliko sehemu yoyote na kuongeza kuwa sio sehemu za ajira rasmi tu bali ni sehemu yeyote ambayo watu wanapata kipato ikiwemo sokoni na kutolea mfano soko linapounguahivyo mkakati huo utaenda kuangazia eneo hilo.

Dkt. ubuguyu ametaja pia sehemu ya tatu ni afya ya akili katika jamii ambap ndio ombwe kubwa kwani taktika jamii unapotaja afya ya akili watu huanza kucheka na kuona magonjwa au shida mbele badala ya kuonekana afya kwa ujumla wake kwani watu wanapowasiliana ni kwamba afya zao za akili zipo sawa.

Hata hivyo Dkt. Ubuguyu alisema  suala la afya ya akili Wizara ya afya imelipa kipaumbele ikiwemo maboresho ya miundombinu kwenye hospitali ya Taifa ya afya ya Akili ya Mirembe pamoja na hospitali za rufaa za mikoa.

“Uwekezaji katika miundombinu na kwa watoa huduma ambapo hivi sasa tumefanyia maboresho makubwa kwenye Hospitali ya Taifa ya afya ya akili ya  Mirembe hospitali za rufaa za mikoa  11 kati ya 28 zinatoa huduma za afya ya akili hasa huduma za kulaza”.Alisema 

Kwa upande kwa kukabiliana na changamoto ya afya ya akili ni utoaji wa elimu  kwa ujumla kwa maana watu waelewe kuhusiana na masuala ya  afya ya akili na si kusubiri kushughulika na watu wenye Magonjwa ya akili.

Aliongeza  kuwa   Wizara ya Afya inayo jukumu kubwa  la kushughulikia afya ya akili pamoja na Wizara ya maendeleo  ya jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu  ambayo inashughulikia na afya ya akili aidha, inayo watu wenye makundi maalumu hivyo kuhakikisha watu hao hawapati changamoto za afya ya akili

Changamoto ya afya ya akili Kitaifa Dkt. Ubuguyu alisema hali ni mbaya na sio tu Tanzania bali dunia nzima na kuongeza kuwa sehemu kubwa ya ukatili imebebwa na sehemu ya malezi kuanzia kwa watoto ambapo makuzi yanakuwa sio mazuri kwani wazazi wamekubwa ‘busy’  kutafuta maisha na hali ya kuchangamana na watu ikiwemo mitandao ya kijamii.

“Uchochoe wa vurugu na matatizo kwenye  jamii  ni ukorofi pamoja wazazi wengi huelekeza watoto kwa kupiga  hivyo ukatili huo humfanya mtoto kujua hayo ndio maisha na hivyo inakua rahisi kuwa na ukatili kwa jamii tofauti na zamani ambapo watoto walikua wakipelekwa kwa babu na bibi zao”.

Dkt. Ubuguyu alitoa wito wa jamii na  familia kwa ujumla kuacha tabia ya ukatili kwa watoto na hivyo kujenga mazoea ya  kukaa na kuongea pamoja kama  familia kwani dunia imebadilika.



Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI