Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akikata utepe kuashiria ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kito cha michezo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi huo eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo,akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Uwanja wa Gofu, Hoteli ya nyota tano na kituo cha michezo katika eneo la Jeshi Ihumwa leo Juni 28,2022 Jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Generali Venance Mabeyo amezindua jengo la uwekezaji Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la kujenga Taifa SUMAJKT na ameweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa hotel ya nyota 5,uwanja wa mchezo wa gofu na kituo cha michezo jijini Dodoma inatakayoghalimu kiasi cha shilingi bilioni 62.8.
Pia amewataka wanajeshi kuendelea kushirikiana na wananchi katika burudani na kupata huduma mbalimbali na kwamba kujiweka karibu kwa kuwa wao wanatokana na wananchi hao.
Hayo ameyayasema Jijini hapa katika hafla hiyo amesema jiji hilo linahitaji miundombinu mingi ya kisasa ili kuweza kukidhi mahitaji mbalimbali kama matarajio mbalimbali ya makao makuu ya nchi ambapo miundombinu hiyo itae ndelea kupunguza uhaba wa miundombinu katika nchi mfano hotel kubwa za kisasa.
"Nawahamasisha wadau wa maendeleo kuendelea kujenga na kuweka miundombinu kama vitega uchumi ili kupunguza uhaba wa miundombinu na uhaba wa ajira kwa vijana wa Dodoma, ameongeza.
“Miundombinu kama hii itakuwa chanzo cha mapato kwa mamlaka za jiji la Dodoma na uchumi wananchi na ujenzi wa huu utakapoanza utatoka ajira kwa vijana wa Dodoma," ameeleza.
Aidha ameazitaka mamlaka mbalimbali za serikali kuendelea na ushirikiano ili kuliwezesha jiji kuwa na miundombinu ya kutosha na yakisasa kwa lengo la kuwa na hadhi ya makao makuu ya nchi katika karne ya 21.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mradi huo Brigedia generali Hassan Mabena ametoa taarifa juu ya mradi huo na kusema eneo hilo lina ukubwa wa hekari 523 ambapo ni wa pili kujengwa na jeshi la ulinzi.
"Huu ni muendelezo wa kuthamini na kutambua umuhimu wa michezo na afya ya watanzania baada ya ule wa Lugalo gofu Dar es salaam, amesema.
Ameongeza kuwa lengo lao ni kujenga viwanja 9 vya mwanzo na mpaka sasa tayari viwanja viwili,kiwanja namba 1 ndicho kimewekewa jiwe la msingi.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu General George Waitara alisema kuwa uwanjo huo ni uwanja muhimu sana upo katika eneo zuri na jiji la Dodoma bila kuwa na uwanja huo litakuwa halijakamilika ili kuendana na hali ya majiji na makao makuu ya taifa.
“naamini nchi mbalimbali zikisikia kuwa Dodoma kunauwanja wa gofu watakuwa wanakuja kucheza na jiji la Dodoma litakuwa na wageni wakila aina,naamini hata wakazi watakuwa miongoni mwa wageni watakao kuja kucheza na tuaache imani ya kusema kuwa huu ni mchezo wa watu wenye kipato kikubwa,’’alisema Waitara.
Aidha alisema kuwa matamanio yake ni kwamba kila kanda ya jeshi iwe na uwanja wa gofu na huo utaongeza chachu pia kutoa mchango kwa mchezo wa gofu hapa nchini.
Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa gofu Tanzania Chris Martine aliwataka maafisa waliopo Dar es salaam na Dodoma ambapo viwanja vya gofu vipo waweze kuwajengea mapenzi ya mchezo wa gofu kwani wakianza utotoni kutawajengea mapenzi zaidi hata watakapo kuwa watu wazima.
Amesema kwa upande wa Dodoma ilikuwa ikiuliziwa mara nyingi ni kwa muda gani uwanja wa gofu utajengwa hata baadhi ya watumishi kutoroka na kwenda Dar es salaam siku ya weekend kwaajili ya kucheza gofu.
0 Comments