WAZIRI SIMBACHAWENE AWATOA HOFU WATU WENYE ULEMAVU ZOEZI LA SENSA


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene,akizungumza leo Juni 29,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga. ,akizungumza wakati wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.


Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa,akizungumza wakati wa  Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.


Mwenyekiti Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Bw.Ernest Kimaya ,akizungumza wakati wa  Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene, (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lililofanyika  leo Juni 29,2022 jijini Dodoma 

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene, amesema kuwa lengo la kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu  na Makazi kwa watu wenye ulemavu sio kujua idadi yao bali serikali iweze kupata takwimu zao na  kupanga mipango yake kuhusiana na watu hao ya kimaendeleo.

Hayo ameyasema jijini hapa Juni 29,2022  wakati akifungua Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022  kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Amesema kuwa lengo la kongamano hilo serikali ni kutaka watu hao kuwa kipaumbele kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi na kwamba mkusanyiko wao unaashiria ni ushindi na wapo tayari kuhesabiwa. 

“Tunatarajia kuona matokeo makubwa kutoka kwenu kwas
kwa kuwa Sensa ni ya Watu wote na hii itawaongezea ufahamu kuhusu zoezi hili hivyo watu wote watapata fursa ya kushiriki,"  Simbachawene.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Ummy Ndalienanga
ameeleza kuwa wao watu wenye ulemavu watashiriki kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi itakayofanyila Agosti 23 mwaka huu huku  akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu na kuwaamini katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema watahakikisha wale waliopata nafasi mbalimbali za uongozi wanafanya kazi kwa bidii ili wasimuangushe  Rais Samia ili  aendelee kuwaamini wengi zaidi kwani wanaweza.

" Nampongeza Rais Samia kwa kutujali sisi wenye ulemavu ameonyesha kutupenda na tunamhakikishia kuwa tutaendelea kumpa ushirikiano tunaomba aeendelee  kutuamini na kutoa nafasi mbalimbali za uongozi na sisi tunamhakikishia kuwa hatutamuangusha tutafanya kazi kwa bidii,"amesema.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana,Ajira,Kazi na Watu wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema Rais Samia ametoa kiwanja Mtumba hapa Dodoma chenye thamani ya shilingi milioni 36 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya shirikisho la chama Cha watu wenye ulemavu.

Amesema Rais Samia amekuwa akijipambanua katika kujali kundi hili la watu wenye ulemavu kwa kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo kuhakikisha haki zao zinalindwa, kutoa kipambele kwa watu wenye ulemavu katika fursa mbalimbali zinazojitokeza nchini.

 "Rais Samia amesisitiza pia kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawezwashwa kiuchumi katika kuhakikisha wanapata mikopo kwa ajili ya kendesha shughuli mbalimbali za Kilimo, ufugaji na biashara," amebainisha.

Ameongeza kuwa Elimu jumuishi kuhakikisha ngazi zote watu wenye ulemavu wanapata  na Taya katika kuhakikisha hilo tayari Rais Samia ametoa fedha kwa ajili ya kujenga mabweni 50 katika Halmashauri 50 lengo ni kuhakikisha wanapata elimu Bora.

Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa amesema lengo la kuandaa kongamano hilo ni  kupeana misingi na faida ya zoezi la sensa ya watu na makazi kwa watu wenye ulemavu.

Amesema tangu maandalizi ya sensa yalipoanza mwaka 2018 serikali ilianza  kushirikisha kundi la watu wenye ulemavu katika hatua mbalimbali lengo ni kuhakikisha nao wanahesabiwa na Taifa linakuwa na takwimu sahihi la kundi hilo.

"Katika ya sensa ya watu na makazi ya  itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu  tumeweka maswali ya kutosha ambayo yatasaidia kupata takwimu sahihi   zitakazosaidia serikali kupanga mipang ya maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla,"ameeleza.

Ameongeza kuwa sensa  hiyo ni ya sita  kufanyika hapa nchini lakini chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan itahusisha kwa kiasi kikubwa watu wenye ulemavu kuliko sensa zilizopita.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema suala la sensa kama mkoa wameanza kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika masuala mbalimbali.

Ameeleza kuwa sensa zilizopita hawakuona mjumuisho wa watu wenye ulemavu kama ilivyo na elimu hiyo italeta mageuzi makubwa katika sensa ya mwaka huu.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha watu wenyeulemavu  Tanzania Diwanai amesema takwa la Rais Samia la kutaka sensa ya watu na makazi kushirikisha watu wenye ulemavu.

Amesema kongamano hilo linaenda kufungua uelewa kwa watu hao ili wakahamasishe watu wengine  kwa ajili ya kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika hapa nchi Kwa lengo la kutafuta takwimu sahihi kwa mipango ya serikali.

"Tunatarajia baada ya kupata uelewa tutaenda kuhamasisha watu wengine  ili wajitokeze kuhesabiwa katika sensa ya mwaka huu na sasa kuna timu ya  uhamasishaji inayopita katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar inaendelea na tumefurahishwa kuona   watu wenye ulemavu wameshirikishwa katika timu hii na wanafanya kazi nzuri,"amesema.



Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU