Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof Adolf Mkenda akizungumza Jijini Dodoma wakati akifunga maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi yaliyoanza June 7,2022 Katika uwanja wa Jamhuri.
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa serikali bado inahitaji kuimarisha vyuo katika sekta ya utalii na kuwekeza kwa lengo la kuvisogeza mbele katika sekta hiyo
Hayo ameyasema jijini Dodoma Juni 13, wakati akifunga maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi amesema hayo ni maagizo ya Rais Samia suluhu Hassan katika hotuba yake ya kwanza alivyoshika dola ya kupitia sera na mitaala ya elimu, kuongeza, kuiandaa na kuweza kutoa huduma bora Kwa kwa muhitimu ili aweze kujiajiri na kuajirika.
Waziri Mkenda amesema kuwa mitaala ya shule za awali, msingi na sekondari wameshaipitia na kwamba kwa upande wa vyuo vya kati vipo vya aina nyingi maudhui tofauti tofauti hivyo ni lazima kutekeleza maagizo ya Rais Samia kupitia mitaala hiyo kuongeza ubora, Ujuzi kuhakikisha wahitimu wanaajiriwa na wanajiajiri.
"Wizara ina kazi kubwa vyuo ni vingi maudhui mbalimbali hii kazi ya kupitia mitaala ya elimu shule za awali msing na na sekondari inaenda vizuri. Tulikusaya maoni ya upitishaji wa mitaala zaidi ya laki moja," amesema Prof. Mkenda.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa bado wanakazi ya kuongeza ubora wa elimu hapa nchini ambapo maagizo ya Rais Samia ya kuongeza ujuzi ni mahitaji ya wazazi wa watoto wanaosoma huku akitole mfano Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dodoma kuwa kinafundisha ukarimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi na Ufuatiliaji Rasilmali kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Waziri Salum
ameaema kuwa maonyesho hayo yana faida kubwa kwa Mamlaka hiyo na kwamba inajukumu la kusimamia mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF).
Amesema mfuko huo unawapa ufadhili vijana na akina mama wa kujifunza usindikaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na kukuza mambo ya utalii na Nishati na kuweza kujiajiri wenyewe Kwa kuwa ni tatizo la ajira sio tu kwa Tanzania bali Afrika.
" Hapa tumekuja na wanufanika wa ufadhili wa mafunzo wa mfuko wa SDF kuna akina dada ambao wanasindika waini, kijana kutoka Lindi ambaye amekuja na matofali ya kuugandamana " Inter Lock" na huyu mama ambaye naye amekuja na bidhaa zake alizosindika wote hawa tayari wanamasoko hapa nchini ," amesema.
Ameongeza kuwa hao ni wachache waliofika katika maonyesho hayo kutokana na ufinyu wa maeneo na kwamba TEA tayari imeshawapa mafunzo ya ujuzi vijana zaidi ya 5000.
Mkurugenzi huyo amesema Watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa TEA ni mamlaka ya serikali hivyo inapambana kuhakikisha vijana na akina mama wanapata ujuzi ili kujikwamua kiuchumi.
Ameeleza kuwa vijana wengi wanaomaliza vyuo wanakimbilia kutafuta ujuzi wa kujiajiri na kuwaajiri wenzao huku akisema kwamba anaamini katika mabadiliko ya mitaala ya Elimu watawekeza katika ujuzi.
0 Comments