TEA KUPITIA MFUKO WA SDF YAWAINUA VIJANA KIUCHUMI


 

Mnufaika na mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), Yusuf Mchola akiwaelezea baadhi ya wanafunazi waliotembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), katika Monyesho ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yanayoendelea katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa
zinazopatikana kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),chini ya Mfuko wa Kuendeleza ujuzi (SDF),ili kuanchana na malalamiko ya kukosa ajira na kuanza kuilaumu serikali.

Hayo yamesemwa Juni 12,2022 jijini  Dodoma  na mnufaika wa mfuko wa SDF kupitia chuo cha Maendeleo ya Wananchi Chilala kilichopo mkaoni Lindi katika Maonyesho ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo Stadi (NACTVET),yanayoendelea katika uwanja wa Jamuhuri,Yusuf Mchola amesema kuwa  baadhi ya vijana hawajiamini kuchangamkia fursa pindi zinapotokea ambazo zinazodhamiwa na serikali.

Amesema kuwa chuo cha Maendeleo ya Wananchi Chilala ni moja ya wanufanika wa SDF ambao umelenga zaidi kuwaelisha vijana kupitia ujuzi ili waweze kujiajiri wenyewe huku akisema kuwa alipata ujuzi wa kufyetua matofali ya kufungamana ambayo hayana gharama vkubwa katika ujenzi wake.

Mchola amesema kuwa matofali hayo yanatumia kiwango kidogo cha saruji lengo ni kumfanya mwenye kipato cha chini kuweza kujenga nyumba nzuri Kwa gharama nafuu hasa Kwa waliopo vijijini.

Ameongeza kwamba faida ya ujenzi wa matofali hayo ni rahisi kwa kuwa ni wa kupachika tofauti na ule wa kawaida ambao unatumia udongo au saruji  wakati wa kujenga.

Mchola ameeleza kuwa faida nyingine ya matofali hayo ni kwamba mfuko mmoja wa saruji unatoa matofali 85 hadi 110 na inategemea na aina ya mchanga utakao tumika.

CHANGAMOTO

Amesema changamoto ni baadhi ya watu kuwa na  uelewa mdogo  bado hawaamini moja kwa moja kwenye aina hiyo ya ujenzi jambo ambalo linakuwa ni kikwazo kwao.

Mchola amefafanua changamoto nyingine ni ukosefu wa mashine ya kufyetulia matofali hayo ambayo inauzwa kuanzia laki sita na kuendelea ambapo kwa Sasa wanaaziama kupitia mfuko wa SDF baada ya kupata mafunzo.
 
"Nilipata haya mafunzo ya kutengeneza matofali ya kushikamana katika Chuo Cha Maendeleo cha wananchi Chilala kilichopo Lindi kupitia Mamalka ya elimu Tanzania chibi ya   ufadhili WA mfuko WA kuendeleza ujuzi (SDF)," amesema.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo walipata wanafunazi zaidi ya 400 wenye fani tofauti tofauti katika chuo hicho ambapo wao waliunda kikindi cha watu 10  ambao wapo katika ujunzi na kuanza kufyetua matofali hayo.

" Katika kikundi chetu tuna watu wa ujenzi, wa kupaua, kuweka Maru maru, wapaka rangi ili iwe  rahisi kupata oda za matofali  na lengo letu kubwa ni kuteka Soko la ujenzi," amesema Mchola.

TEA imepewa jukumu  na Wizara ya Elimu, Sanyansi na Teknolojia la kusimamia mfuko wa Kuendeleza Ujuzi ( SDF), ambao unatoa ufadhili kwa Taasisi zinazolenga kutoa mafunzo ya kuendeleza ujuzi katika sekta sita za kipaumbele zinazoratibiwa na programu ya (ESP J).



Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU