VETA ARUSHA YAJIKITA KUTANGAZA UTALII WA NDANI NA NJE YA NCHI



Mbunifu, Ushonaji na Teknolojia ya  Mavazi Kitengo cha Ushonaji kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Arusha Mwalimu Elizabeth Luwongo, akionyesha baadhi ya bidhaa ambazo wanawafundisha wanafunazi katika maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Jamuhuri  jijini Dodoma.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),imekuwa ikitoa mafunzo ya vitu mbalimbali kulingana na mazingira mahali husika kwa lengo la kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi kwa kununua bidhaa zilizotengenezwa kiasili.

Hayo yamesemwa hivi karibuni katika  maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi  na Mbunifu, Ushonaji na Teknolojia ya  Mavazi Kitengo cha Ushonaji kutoka Veta Arusha Mwalimu Elizabeth Luwongo, amesema kuwa wanafundisha vijana kushona nguo aina  mbalimbali za kike na kiume pamoja na kubuni bunifu mpya ambazo ni za asili.

Amesema wanapo wafundisha vijana wanaojikita zaidi katika kuweka thamani ya vitu ambayo vinapatikana vya kiutamaduni kama vile Shanga na kwamba  wanafikiria zaidi ili wageni wanapofika  nchini kuangalia bidhaa zinazozalishwa  na vyuo vya veta kupitia wanafunazi hao kwa usimamizi wa walimu wao waweze kuvutiwa na kununua.

"Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan ameweka fedha nyinyi katika kuwekeza kwenye kutangaza utalii wa Tanzania, sisi kama washonaji lazima tutengeneze bidhaa nzuri na bora ambazo zinatazamika na kutangaza utamaduni wetu," amesema Mwalimu huyo.

Ameongeza kuwa wageni watakavyonunua bidhaa na kwenda nazo nchini mwao watautangaza utalii wa Tanzania hivyo itawavutia  watalii wengi zaidi kuja nchini si kwa kununua bidhaa  hizo tu bali kwenda kuangalia wanyama.

Mwalimu Luwongo amesema kuwa wanafunzi wao wanapata dhana halisi ya ubunifu sio kushona tu bali kuongeza thamani ya mavazi au vitu ambavyo wanatengeneza.

" Nawasisitiza wananchi wawalete watoto wao kuja kusoma veta kupata ufundi ambao ni mahiri na watakuwa na dhana halisi ya kuwa wabunifu pamoja na  kutangaza utamaduni wetu ili usife," amesema.  

Akizungumzia mwimamko wa Watanzania kutumia bidhaa za ndani ameeleza kuwa upo katika Mkoa wa Arusha ambapo kuna watalii wa ndani na nje ya nchi.












Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI