Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Daktari Jimmy Yonazi akizungumza wakati akufungua kikao kazi cha uchambzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa na Kimataifa kilichofanyika jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Daktari Jimmy Yonazi amewataka wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano nchini kukuza maarifa na kuwa na uchumi shindani wa kidijitali.
Dk. Yonazi ametoa kauli hiyo Leo jijini Dodoma katika kikao kazi cha uchambzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa na Kimataifa ambapo wizara ya mawasiliano imekusudia kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa ili kuwa nchi yenye fursa nyingi ili nchi nyingine nazo zije kujifnza Tanzania.
Sanjari na hilo Dk.Yonazi ametaka Kila Mtumishi atambue jukumu lake na siyo kwenda ofisini na kurudi nyumbani tu huku akiwasisitiza kufanya kazi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kimataifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Mulembwa munaku amesema kuwa watatekeleza maagizo ya serikali ili kuongza ajira pamoja na pato la Taifa.
" Haya tuliyoelekezwa na serikali tutaenda kuyatekeleza na kuyafanyia kazi Kwa weledi kwa lengo la kuhakikisha Pato la Taifa linaongezeka na kupitia ajira," ameeleza.
0 Comments