LAINI ZA SIMU NCHINI ZAFIKIA MILIONI 58.1


Na Asha Mwakyonde,Dodooma

SEKTA ya Mawasiliano ya Simu nchini imeendelea kukua hadi kufikia Septemba 2022 ,kulikuwa na laini za simu za milioni 58.1, idadi hiyo inahusisha laini zinazotumiwa na watu pamoja na zinatotumiwa kwa ajili ya Mashine (M2M).

Pia takwimu zinaonesha mikoa mitano  inayoongoza nchini kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika (Active SIM-Cards),hadi kufikia Septemba mwaka huu ni Dar es Salaam laini milioni 9.7, Mwanza milioni 3.7, Arusha 3.4, Mbeya 3.08 na Tabora 3.06.

Akizungumza jiijini Dodoma Novemba 3,2022  wakati akitoa taarifa ya utekelezaji  wa majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA), Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo ,Dk. Jabir Bakari  amesema kuwa wanawatoa huduma sita kwenye soko lao ambao ni Airtel,Vodacom,Halotel, Ttcl ,Tigo na Smile.

Dk. Bakari ameeleza kuwa mgawanyo wa asilimia za soko kwa  kila mtoa huduma ni kwamba Vodacom asilimia 30, Airtel asilimia 28, Tigo asilimia 26, Halotel asilimia 13, Ttcl asilimia 3 na Smile asilimia 0.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa takwimu zinaonesha matumizi ya Intaneti  yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka milioni 29 hadi kufikia 31. 12 mwezi  Septemba mwaka huu.

"Mwelekeo wa ongezeko la watumiaji wa Intaneti linaonesha kulikuwa na utumiaji takriban asilimia 17 kila mwaka  katika kipindi cha miaka mitano ambapo mwaka 2017 kulikuwa na watumiaji milioni 16.10 na mwishoni mwa mwaka 2021 waliongezeka na kufikia milioni 29.10," amesema.

Amefafanua kuwa ongezeko la matumizi ya Intaneti limechangiwa na matumizi ya kiswahili  na kwamba maudhui  hayo kwenye Intaneti yanaongezeka kwa kasi na program tumizi  (applications), kwa lugha ya kiswahili  nazo zimeongezeka.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU