MAGANDA YA MAYAI YANAVYOSAIDIA KUUZA VIJIDUDU KATIKA MIMEA


 Mkulima Magreth Malogoakitoa elimu kwa wakulima wenzake.



Afisa  kilimo wa Wilaya ya  Chamwino Living Kilawe akizungumza na wakulima.
Na Asha Mwakyonde, Dodooma

WAKULIMA wameshauriwa kutumia kilimo ikolojia ikiwemo mbegu bora, Mbolea za asili lengo likiwa ni kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, Lengo na kutengeneza rutuba ya udogo ili kumsaidia  mkulima kuongeza uzalishaji.

Ushauri huo umetolewa  katika mkutano wa Wadau wa Kilimo ‘’Kilimo Ikolojia kwa Maisha na maendeleo endelevu’’ ulioandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Action Aid Tanzania uliofanyika Kijiji cha Msanga Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Novemba  22, 2022.

Akitoa elimu kwa wakulima wenzake  Mkulima Magreth Malogo amesema katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi wao kama Jukwaa la Vijana Wilaya ya Chamwino wameweza kubuni maganda ya Mayai  ya kuku yanayotumika kufukuza vidudu kwenye mimea.

‘’Unayachukua maganda ya mayai unayatwanga kwa njia ya kiyenyeji kwenye kinu, au unayafikicha ukishamaliza kuyatwanga unaenda kumwagia kwenye mimea yako, ile harufu yake  inasaidia kuzuia wadudu wasumbufu,’’ameongeza.

‘’Lakini pia ukiyatwanga u
kutokana na ardhi yetu hii imeathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi, katika kuirudisha ardhi ikae sawa maganda yahaya ukiyatwanga na ukaenda kumwaga shambani kwako inapunguza ACID ya udongo,’’ amesisitiza Malogo.

Mbali na hayo wameendelea kushauri kuboreshwa kwa mashamba darasa , kutenga bajeti ndani ya vyanzo  vya mapato ndani ya halmashauri kununua kipimia udongo ili kusaidia kujua afya ya udongo inayotakiwa.

Naye mgeni  rasmi katika Mkutano huo, Diwani Mstaafu kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Chamwino Samweli Kaweya amewaasa wakulima kutumia dhana,mbolea, madawa ya asili , katika suala nzima la kilimo.

Kwa upande wake afisa  kilimo Chamwino Living Kilawe amesema  Wilaya ya hiyo  imekuwa ikikubwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuwa na joto kali, mvua kutonyesha na  ukame wa muda mrefu hivyo wanaendelea na jitihada za kupambana na changamoto hizo.

Ameongeza kuwa  Wilaya hiyo imegaramia upatikanaji wa hati ya Shamba la Ekari 8000 katika kijiji cha Membe ambapo bwawa kubwa la kuvunia maji kwaajili ya shughuli za mifugo na kilimo, ujenzi wake unaendelea na kwamba takriban bilioni 11.96 zitatumika.

Naye Mratibu wa Habari, mawasiliano na teknolojia kutoka Shirika la Action Aid amesema lengo la kuandaa Mkutano huo wa wadau ni kuwakumbusha wananchi wa Wilaya hiyo na Vijiji vyake juu ya umuhimu wa kilimo ikolojia kuelekea msimu wa  kilimo unaokuja  2022/2023 .

‘’Kilimo ikolojia  nyezo ya wakulima katika kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, katika Mkoa wa Dodoma kwa ujumla tunaona kunachangamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia ya nchi ndio sababu ya kuwa na  msukumo na mpango wakuhakikisha elimu hii ya kilimo ikolojia inawafikia ili kurejesha hali ya kilimo na kuwafanya wananchi wawe na maendeleo endelevu,’’amesema Hassan.




Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI