NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM
MSANII wa vichekesho kupitia video fupi za mitandaoni Abdul Khamis maarufu Mipazo Artist amewaomba wadau kumsapoti vitendea kazi vikiwamo kamera, kompyuta mapakato (laptop), ili aweze kukiendeleza kipaji chake ambapo kwa sasa anatumia simu ya mkononi.
Akizungumza na Ihojo Media msanii huyo amesema kuwa anaipenda sanaa hiyo ambayo anaamini itamsaidia katika kukuza kipato chake ikiwa ni sehemu ya ajira yake ameeleza kuwa changamoto kubwa anayopitia ni katika uandaaji wa kazi zake.
"Nilianza sanaa hii ya kutengeneza video fupi za vichekesho mtandaoni tangu mwaka 2019 ,nilikuwa nikiandaa kazi zangu kwa kutumia kamera ya simu na kuzitengeneza kwa kutumia simu hii ya mkononi," ameongeza.
Umaarufu wangu na video zangu ulianza kuvuma baada ya kuwatengezea vichekesho watu maarufu kama wasanii wa muziki nchini wao wanazifurahia na kuzichukua wanaziweka kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram Watu wengi Walianza kunijua na kuanza kunifuatilia kwenye mitandao yangu ya kijamii na kujipatia wafuasi wengi zaidi," amesema Mipazo Artist
Mipazo Artist ameeleza kuwa pamoja na changamoto katika sanaa hiyo lakini hakuwahi kukata tamaa ambapo jitihada zake na uvumivu kwa sasa amefikia hatua ya kukodi kamera kubwa kwa ajili ya kazi zake huku akisema hiyo ni moja ya mafanikio makubwa kwake.
"Naomba wadau na wafuatiliaji wa kazi Zangu muendelee kunipa sapot yenu kwa kazi zangu ninazozifanya hivyo kwa yeyote anaeguswa na changamoto zangu kwa kunisaidia atanipata kupitia mitandao ya kijamii kwa jina la Mipazo Artist," ameongeza
Nawaomba ambao hamjanifollow kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii Tafadhalini nawaomba nawaomba wanifollow.
0 Comments