NA ASHA MWAKYONDE, DODOOMA
CHUO cha Taifa Cha Usafirishaji Tanzania (NIT),kimesema kuwa
kina kozi kwa ajili ya kusaidia, kufundisha wataalamu wa reli na zile zenye viashiria na kozi hiyo ambazo ni program 22.
Pia Chuo hicho kimenunua ndege mbili za mafunzo zenye injini moja ambazo zimegharimu shilingi bilioni 4 na kwamba zinatarajiwa kuwasili nchini Januari mwakani.
Akizungumza jiijini Dodoma Novemba 3,2022 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Chuo hicho Mkuu wa Cha NIT Profesa, Mhandisi Zacharia Mganilwa,amesema kuna njia kuu tano za uchukuzi na Usafirishaji ambazo ni usafiri wa barabara, reli ,wa anga, kwa njia ya maji na kwa njia ya mfumo wa mabomba.
Prof. Mhandisi Mganilwa amesema
Wataalamu hao wanawafundisha kwenye njia hizo na.kwamba wapo kwenye makundi matatu ambao ni wataalamu wa uhandisi wa miondombinu ya Usafirishaji kwa kila njia ya usafirishaji, wa barabara ,wahandisi wa vifaa vya reli, wahandisi wa maji na kwenye anga wahandisi wa ndege, wahandisi wa mitamo ya mabomba na wahandisi wa operesheni.
Ameongeza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo,kufanya utafiti na kinatoa ushauri wa kitaalamu huku akisema kwa Sasa kipo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
Prof, Mhandisi Mganilwa ameeleza kuwa katika kutekeleza majukumu yake chuo kwa sasa kina program zinazoanza Stashahada na Astashahada 25, shahada za kwanza 15, Shahada za uzamili 3 na Postgraduate
Diploma 9 pamoja na wafanyakazi 360 na kwamba idadi hiyo inaongezeka kila mara.
Ameeleza kuwa katika udahili wa mwaka wa masomo ulioisha 2021)2022 chuo hicho kulikuwa na wanafunzi 13,000 huku akisema chou hico ni cha kisekta katika serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kina miradi mikubwa ya kimkakati.
Mkuu huyo amesema Chuo hicho ni moja ya vichache ambavyo vimepewa jukumu la kuandaa rasilimali watu ili uwekezaji uwe wa manufaa, Chuo kinaendesha vituo viwili vya umahiri, Kituo Cha Umahiri Cha Mafunzo ya Taaluma za Usafiri wa Anga na Operesheni za Usafirishaji (Center of Excellence in Aviation and Transport Operations),iliyoanzishwa kwa mradi wa Benki ya Dunia unaoitwa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (Mradi wa kukuza ujuzi na muingiliano wa kikanda katika Afrika Mashariki.
"Kituo hiki cha Umahiri kimeanzishwa kwa fedha za Benki ya Dunia kiasi cha USD 21,250,000 Sawa na takriban TZS Bilioni 49," amesema Prof. Mhandisi Mganilwa.
Ameongeza kuwa katika fedha hiyo upande wa miundombinu ya ujenzi na majengo matano Mabibo na tayari waneshasaini mkataba wa bilioni 21 na kwamba baadae katika mkabata mwingine watajenga majengo mengini mkoani Kilimanjaro
Prof. Mhandisi Mganilwa amesema fedha hivyo pia zitatumika kununua vifaa kwa ajili ya kuwafundishia marubani, wahandisi wa ndege na mahudumu ndani ya ndege.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Mawasiliano Idara ya Habari Maelezo Gerson Msingwa amekipongeza chuo hichojwa kazi zake.
"Safari inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia ya kuwekeza katika uhai wa uchumi NIT inaenda kutuwwzeha katika miradi mikubwa, " amesema.
0 Comments