Na Asha Mwakyonde, Dodoma
MADAKTARI wa Mifugo nchini wametakiwa kuhakikisha wafugaji wanachanja mifugo yao lengo likiwa ni kutokomeza magonjwa yanayoishambulia mifugo ikiwemo ugonjwa wa sotoka na kichaa cha mbwa.
Haya yamesemwa jijini Dodoma Disemba 5, 2022 na Mkurugenzi wa huduma za Mifugo, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa. Hezron Nonga wakati akikabidhi chanjo kwa wataalamu zilizotolewa na chama cha madaktari wa mifugo nchini (TVA),zitakazotumika kuchanja mifugo zaidi ya elfu sita.
Amesema kuwa chama hicho kimetoa chanjo 1100 zenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni tatu lengo ni kuwezesha wananchi wa Dodoma kuwa salama na kuepuka kichaa Cha mbwa pindi wanapong'atwa.
Prof. Nonga amesema suala la chanjo ya mifugo linapaswa kuwa ajenda ili kutokomeza magonjwa ya mifugo kwa asilimia 70 mpaka ifikapo mwaka 2030
ambapo hadi sasa uchanjaji wa mbwa bado upo chini kwa asilimia 45.
"Tanzania kama nchi nyingine zipo kwenye ukanda wa kitropikali ambazo zina joto la wastani zinawezesha vimelea kustawi na kuzaliana kuna mvua na jua kiasi unyevunyevu unaowezesha vimelea ambavyo vinaweza kusababisha maradhi kwa mifugo w kama minyoo fangasi na maradhi mengine," ameeleza Prof. Nonga.
Prof. Nonga ameeleza kuwa Wizara ilichagua magonjwa 13 kama magonjwa ya kipaumbele ikiwemo ya kichaa cha mbwa na kwamba mpango wa serikali ni kutomeza ugonjwa wa sotoka ya mbuzi, kondoo pamoja na kichaa cha mbwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini TVA Profesa Esron Karimuribo amesema wataendelea kushirikiana na serikali kwa kuzalisha chanjo ya mifugo ili kumaliza magonjwa ya mifugo.
“Tunaanza chanjo kesho kwa jiji la Dodoma pembezoni kidogo mwa jiji la katika maeneo ya nala mbalawala lakini pia tutakuja kutoa hadi jiji lengo likiwa ni kutokomeza kabisa kichaa cha mbwa” amesema Karimuribo.
Naye Mwakilishi wa chama cha madaktari wa mifugo Jumuiya ya Madola Profesa. Sharadhuli Kimera amesema wao kama madtari wameona kuna haja ya kuchangia kuboresha chanjo ya kichaa cha mbwa lengo ni mpaka ifikapo mwaka 2030 kuwe na maambukizi sifuri ya kichaa cha mbwa.
“Tmekabidhi chanjo hizi 1100 za kichaa cha mbwa na magonjwa ya mapele ngozi kwakuwa sisi tunaelewa ni wapi panahitaji nguvu zaidi,"amesema Mwakilishi huyo.
Amefafanua kuwa shirika la afya za wanayama wameweka lengo la kuondoo kichaa cha mbwa cha binadamu kwa maambukizi sifuri na kwamba ugonjwa huo unaathiri ngozi ya wanayama kwa dozi hizo itasaidia kutoa motisha kwa wafuagaji kujali masilahi ya wafugaji hao.
Chanjo hiyo imezinduliwa katika tarafa za Nala na Mbalawala ambapo dozi 4000 zitatolewa kwa mbuzi na kondoo ili kuwakinga na ugonjwa wa sotoka.
0 Comments